Home » » DUNIANI KUNA MAMBO: AJINYONGA BAADA YA KUDAI DAWA YA KUJIKINGA NA KIFO KUISHA NGUVU

DUNIANI KUNA MAMBO: AJINYONGA BAADA YA KUDAI DAWA YA KUJIKINGA NA KIFO KUISHA NGUVU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Na  Walter Mguluchuma
  Katavi yetu Blog
Mkazi wa Kijiji Cha Igagala Wilaya ya Mpanda  Juma Sadi(50)  amejinyonga hadi kufa kwa kutumia kamba ya chandalua  baada  ya kudai dawa  za kienyeji  alizokuwa  amekunywa za kumzuia  asife na  mapema kuishiwa nguvu.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Igagala  Athumani  Juma  alisema  tukio  hilo  lilitokea  hapo juzi  majira ya saa tano na nusu  jirani na nyumba aliyokuwa akiishi  marehemu.
 Alisema  marehemu kabla ya tukio  alimweleza  shememeji  aitwaye  Tanu  Kabwe kuwa siku hiyo ya juzi  lazima afe  kwakuwa  aliwahi kumeza dawa za kienyeji(Mpigi)  vipande vitatu  ambayo  ilikuwa  ikimkinga asife na  mapema na  alikuwa ameisha vitapika  vipande viwili  vya dawa hizo hapo awali na siku hiyo  ya  juzi alikuwa ametapika(mpigi) yake ya mwisho hivyo hakuwa tena na kinga yoyote.
 Na  alimtaka shemeji yake ambae muda huo walikuwa nae kwenye  kilabu cha pombe  za kienyeji  waende nae hadi nyumbani kwake ili akamkabidhi familia yake  kwani yeye  ilikuwa lazima  afe siku hiyo.
Mwenyekiti huyo wa kijiji alieleza shemeji  yake alipuuzia  maneno hayo hari ambayo ilimfanya  marehemu aondoke kwenye eneo hilo lililokuwa likiuza pombe ya kienyeji na kuelekea nyumbani kwake ambapo alikuta mkewe na kumwambia  amwandalie uji ili anywe kwani alikuwa akisikia njaa .
 Wakati mkewe akiwa anaendelea  kuandaa uji  marehemu alimwaga mkewe kuwa anatoka nje  kwenda kufungia mbuzi na alitoka huku akiwa ameshika kamba ya chandalua mkononi mwake.
Alisema  marehemu  hakurejea tena ndani hadi  majirani walipomwona akiwa amejinyonga hadi kufa huku akiwa  amejifunga kipande  cha kamba ya chandalua  akiwa juu ya mti wa mwembe uliokuwa jirani na nyumba yake.
Majirani wa eneo hilo baada ya hapo walitowa taarifa kwa uongozi wa Serikali ya Kijiji ambao nao walitowa taarifa  kwa jeshi la polisi ambao walifika kwenye eneo hilo na kisha mwili wa marehemu ulifanyiwa uchunguzi wa Kidaktari na kukabidhiwa ndugu kwa mazishi.
Shemeji wa marehemu  Tanu Kambwe  alisema mazishi ya shemeji yake yanatarajiwa kufanyia leo yaani jana Kijijini hapo katika makabuli ya Igagala.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari amethibitisha kutokea kwa  kifo cha mtu huyo na jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi zaidi.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa