Home » » MAUAJI YA WATU WATATU HUTOKEA KILA MWEZI WILAYANI MELELE- MKUU WA WILAYA

MAUAJI YA WATU WATATU HUTOKEA KILA MWEZI WILAYANI MELELE- MKUU WA WILAYA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter Mguluchuma
 Katavi yetu blog
  Matukio  matatu  ya watu kuuwawa  hutokea kila mwezi Wilaya Mlele Mkoani Katavi  kwa kukatwa  katwa na mapanga katika maeneo  wanayoishi  Wafugaji.
Hayo yalisemwa hivi karibuni na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Kanali msitaafu Issa Njiku  wakati alipokuwa akisoma  taarifa ya Serikali ya Wilaya ya Mlele   kwa Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi  Wiliam  Ole  Nasha  kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mlele.
 Alisema  matukio ya mauwaji yamekuwa yakijitokeza  mara kwa mara  Wilayani hapo  ni  mauwaji ya watu  katika maeneo  ya wanako ishi Wafugaji wa mifugo ya Ng’ombe.
 Aliyataja maeneo  ambayo mauwaji hayo yamekuwa yakitokea ni  katika  Tarafa   za Mpimbwe na Mamba katika Halmashauri ya Mpimbwe Ndurumo  katika Halmashauri ya Nsimbo na Inyonga katika Halmashauri ya Mlele.
Kanali Njiku  aliemweleza Naibu Waziri  kuwa kila mwezi hutokea  matukio matatu ya watu kuuwawa  kwa kukatwa katwa na mapanga Wilayani humo.
Alisema katika kukabiliana na hari ya matukio hayo  Serikali ya Wilaya  imeweka mikakati ya kuhakikisha  hali ya ulinzi na usalama  Wilayani humo inakuwa shwari.
 Nawameendelea   kusisitiza suala la  polisi jamii katika  katika kila Kata  na  kuwataka Wananchi  wanapowakamata  wahalifu  au majambazi  kutotumia  sheria  mikononi  badala yake wawafikishe wahalifu Polisi  kwa hatua za kisheria.
Naibu Waziri Nasha  aliwataka viongozi wa Wilaya hiyo waakikishe  wanaweka utaratibu   wa kuzia watu kuhamia kiholela   na wahakikshe watu wanao hamia wanafata taratibu  za kisheria.
 Alisema lengo la Serikali sio kuwazuia watu  kuhamia kwenye maeneo mengine   cha msingi ni watu wanahamia kwenye maeneo wafuate utaratibu na sheria.
 Aidha Nasha aliwataka viongozi wa Wilaya ya Mlele kutenga maeneo ya ardhi kwa shughuli mbalimbali  ili kuepukana na migogoro ya ardhi ambayo imekuwa ikitokea mara kwa mara

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa