Na Walter Mguluchuma
Katavi yetu blog
Manispaa ya Mji wa Mpanda Mkoani Katavi inatarajia kuanza ujenzi wa Barabara zake karika Manispaa hiyo zenye urefu wa kilimeta7.7 kwa kiwango cha Rami zitakazo gharimu kiasi cha shilingi milioni 350.
Haya yalisemwa hapo jana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Selemani Lukanga kwenye kikao cha pili cha Baraza la Madiwani wa Manispaa hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda katika Mtaa wa Ilembo Mjini hapa.
Awali Diwani wa Kata ya Makanyagio Haidari Sumry alitaka kujua Manispaa hiyo inampango gani wa kutengeneza barabara zake kwa kiwango cha rami na zitagharimu kiasi gani cha fedha.
Kufuatia swali hilo la Diwani wa Makanyagio Mkurugenzi huyo alilieleza Baraza la Madiwani kuwa katika kipindi hiki cha mwaka wa fedha wa 2015 na 2016 wanatarajia kujenga Barabara zenye urefu wa kilometa 7.7 zitakazogharimi kiasi cha shilingi milioni 350.
Lukanga aliiambia Baraza hilo barabara zitakazotengenezwa ni katika Mitaa ya Kashauli ,Kawajense Nsemlwa na Mtaa wa Madukani .
Pia aliliambia Baraza la Madiwani kuwa Manispaa hiyo imepata kibali cha kajiri watumishi 195 wa kada mbalimbali ambao watasaidia kupunguza tatizo la upungufu wa Watumishi.
Watumishi ambao wanatarajiwa kuajiriwa ni watumishi wa afya, Waalimu. watendaji wa mitaa, maafisa ugavi ,wahasibu na wakaguzi wa ndani .
Meya wa Manispaa Wiliy Mbogo kwa upande wake alieleza kuwa Manispaa imepanga kuhakikisha maeneo ya Manispaa yanapimwa ili kuufanya Mji kuwa katika mpango mzuri na kuwafanya watu wasijenge kiholela
Pia wanatarajia kuweka alama kwenye maeneo ambayo watu wamejenga kiholela ili waweze kujitambua kabla ya hatua ya kuwabolea na kuwaondoa kwenye maeneo hayo haija anza.
Afisa usitawi wa jamii wa timu salama ya damu Redguarda Mayolwa alieleza jumla ya watu 430 wamejitolea kuchangia damu salama kwa kipindi cha mwaka jana ambapo ziliweza kupatikana uniti 430 za damu salama.
Madiwani
wa Baraza hilo waliomba hatua za haraka zichukuliwe za Manispaa hiyo
kukabidhiwa Hospitali ya Wilaya ya Mpanda ambayo ipo chini ya
Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda ili iwe chini ya Manispaa.
Manispaa hiyo hadi sasa haina Hospitali tangia ilipoanzishwa rasmi mwaka jana na imekuwa ikitumia kituo cha Afya Mwangaza kuwa ndio kinatumika kama Hospitali yao.
0 comments:
Post a Comment