Na Walter Mguluchuma
Katavi yetu blog
tuhuma kumtesa na kumnyanyasa kwa kumnyima chakula, matibabu na huduma za shule na kisha kumfukuza nyumbani kwake kwa kushirikiana na mama yake wa kambo kumnyanyasa mtoto wake aitwae Adamu Ramadhani (17) wanafunzi wa kidato c ya Sekondari ya Kashaulili.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari aliwaambia jana wandishi wa habari kuwa mtuhumiwa alikamatwa hivi karibuni .
Alisema Jeshi la Polisi lilipata taarifa kutoka kwa mtoto huyo kuwa baba yake mzazi anamfanyia vitendo vya ukatili wa kijinsia akiwa anashilikiana na mama yake wakambo aitwaye Joice Sina.
Kamanda Kidavashari alieleza kuwa manyanyaso na ukatili kwa mtoto huyo hivi karibuni baada ya mama yake mzazi kufariki Dunia .
Kabla ya kifo cha mama mzazi wa mtoto huyo walikuwa wakiishi vizuri na kumpa huduma zote muhimu za msingi za kibinadamu,
Kidavashari aliwaeleza waandishi wa Habari ghafla hari ilibadilika ikawa mtoto huyo hapatiwi mahitaji ya chakula na wakati akiugua hapatiwi matibabu chakula na mahitaji yake ya shele
Na wazazi wake waliamua kumfukuza nyumbani na walimtishia kuwa wasimwone anakanyaga nyumbani kwao atafute sehemu nyingine ya kuishi .
Alisema baada ya jeshi la polisi kupata malalamiko kutoka kwa mtoto huyo mwalimwa walimwandikia baba yake hati ya wito ya mkutaka afike kituo cha Polisi cha Wilaya ya Mpanda.
Na alifika kituoni hapo na kutoka kujihami kwa
kufungua taarifa kuwa amepotelewa na mtoto wake ambae ni mwanafunzi wa
shule ya Sekondari Kashaulili na ndipo alipokamatwa na kuwekwa chini ya
ulinzi .
Kamanda Kidavashari alisema mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika na ili aweze kujibu shitaka la kushindwa kutoa huduma mahitaji ya maisha kwa mtoto wake aliye chini ya uangalizi wake na pia jitihada zinafanyika mke wake Joice Sino ilinae aweze kufunguliwa mashitaka kama hayo.
0 comments:
Post a Comment