Home » » JELA KIFUNGO CHA MIAKA 30 KWA KOSA LA KUTAKA KUMBAKA HAWALA YAKE

JELA KIFUNGO CHA MIAKA 30 KWA KOSA LA KUTAKA KUMBAKA HAWALA YAKE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter Mguluchuma
  Katavi
Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi  imemuhukumu  Frenk  Jonas(27) Mkazi wa Mtaa wa Mpanda Hoteli  kutumikia kifungo cha miaka 30 jela  baada ya kupatikana na kosa la kutaka kumbaka hawala yake(Mpenzi wake) mwenye umri wa miaka(17) ambae jina lake limehifadhiwa Mkazi wa mtaa huo.
 Hukumu hiyo ilitolewa juzi na Hakimu Mkazi mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Chiganga Ntengwa  na kuvuta hisia za watu wengi ambao  walikuwa  hawajuwi  kufanya hivyo kuwa ni kosa.
Awali katika kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo  mwendesha mashitaka  Mwanasheria wa Serikali Ongela Malifimbo  alidai kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo  January 9 mwaka huu muda wa saa nane mchana katika eneo la shule ya Sekondari Mwangaza.
Siku hiyo ya tukio  mtuhumiwa alimvizia  njia  msichana huyo wakati alipokuwa akipita katika eneo hilo  na kisha alimtupia  kwenye majani ambayo yalikuwa marefu.
Mwendesha mashitaka  huyo aliendelea kuiambia  Mahakama kuwa baada ya kuwa amemtupia kwenye nyasi aliamvua kwanguvu nguo zake  na kisha alimlalia juu ya kifua chake na wakati huo msichana huyo alikuwa akipiga mayowe ya kuomba msaada
 Alieleza watu waliokuwa karibu na eneo hilo  baada ya kuwa wamesikia mayowe ya  kuomba msaada walifika kwenye eneo hilo na  walikuta Frenk  Jonas akiwa amelalia kifuani msichana huyo  huku akiwa anaangaika kutaka kumvua nguo yake ya ndani na wakati huo msichana akiwa anaendelea kupiga yowe ya kuomba msaada.
Watu walifika kwenye eneo walilazimika kumtoa kwa nguvu  juu ya kifua cha msichana huyo  huku mtuhmiwa  akiwa anawasihi wamuachie  kwani anamfanyia hivyo  kwa vile ni  hawala yake(Mpenzi) na alikuwa amekula hela zake hata hivyo walifanikiwa kumwondoa na kisha walimpeleka  kwenye kituo cha polisi cha Mpanda huku akiwa haja timiza lengo lake la  kufanya tendo la ndoa.
Mshitakiwa baada ya kusomewa mashitaka  alikiri kutenda kosa hilo hapo january  9 mwaka huu katika  eneo la Shule ya Sekondari Mwangaza.
Baada ya mshitakiwa kukiri kosa hilo Hakimu Chiganga Ntengwa  alimweleza mshitakiwa kuwa  kama inayosababu yoyote ya msingi inayoweza kuishawishi Mahakama  impunguzie  adhabu   Mahakama inatowa nafasi hiyo kwa mshitakiwa kujitetea .
Mshitakiwa katika utetezi wake aliomba Mahakama impunguzie adhabu  kwa kuwa  alifanya hivyo kwa vile msichana huyo alikuwa ni mpenzi wake  na alikuwa amekula fedha zake.
Maombi hayo yalipingwa na mwanasheria wa Serikali kwa kile alichodai kuwa  hata kama alikuwa ni mpenzi wake hakutakiwa  kutaka kufanya tendo la ndoa bila lidhaa ya msichana yule.
Hakimu Chiganga akisoma huku hiyo alisema  mshitakiwa  Frenk Jonas Mahakama imemtia hatia kwa kosa la kifungu cha sheria 132(1) sura ya 16   cha marekebisho ya sheria ya mwaka 2002.
Kutokana na kosa hilo  Mahakama imemuhukumu  mshitakiwa kwenda jela kutumikia  kifungo cha miaka 30 jela kuanzi juzi .

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa