Na Walter Mguluchuma
Katavi yetu blog
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza amemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda kuwakamata na kuwafikisha Mahakamani Mwenyekiti wa Kijiji cha Kapamsenga Tarafa ya Karema John Kaleba na Afisa mtendaji wake Michael Shuka
pamoja na wajumbe 19 wa Serikali ya Kijiji hicho kwa kitendo chao cha
kuwauzia adhi watu 52 katika eneo la hifadhi ya msitu na mapito ya
wanyama (Ushoroba)
Mwamlima alitowa agizo hilo hapo jana wakati alipokuwa akitowa taarifa ya tume ya uchunguzi wa migogoro ya ardhi katika vijiji vya Kapamsenga ,Ikaka na Nkungu mbele ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na Usalama wa Wilaya ya Mpanda ofisini kwake mjini hapa.
Alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda kupitia idara ya Ardhi na Mali asili awakamate na kuwafikisha Mahakamani waliokuwa viongozi wa Kijiji hicho ambao wamemaliza muda wao mashitaka ya uvunjifu wa sheria ya wanyama pori ya mwaka 2004.
Hii ni kufuatia uliokuwa uongozi wa Kijiji cha Kapalamsenga kuamua kuuza eneo la Lyamgoloka kwa Wananchi wapatao 52 hapo mwaka 2013 kinyume na sheria za Nchi .
Mwamlima alimwagiza mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Mpanda(ocd) kutowa ushilikiano wa kutosha na kuhakikisha watu hao 21 walioamua kuuza eneo eneo tengefu la ardhi wanakamatwa wakiongozwa na aliyekuwa Mwenyekiti wao John Kaleba na Michael Kishoka(VEO).
Alisema kwa kuwa Serikali ya Kijiji cha Kapalamsenga ilifanya utapeli wa kuwaibia wananchi hao 52 hivyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda aisimamie Serikali ya Kijiji ili watu hao waliokuwa wameuziwa mashamba wapewe mashamba kwenye eneo lililotengwa kwa shughuli za kilimo katika Kijiji hicho.
Alifafanua kuwa tume hiyo ya kufutilia migogoro ya ardhi iliundwa kutokana na kuwepo kwa migogoro mikubwa ya ardhi katika vijiji vya Kapalamsenga, Ikaka na Nkungu-
Alisema tume hiyo imebaini kuwa kamati za ardhi za Vijiji hugawa ardhi zaidi ya mara moja zaidi ya kiwango cha kisheria cha Ekari hamsini na hata bila vikao vya kisheria kufuatwa hivyo kusababisha migogoro.
0 comments:
Post a Comment