Home » » HATARI: AUAWA KWA KWA KUKATWA NA MAPANGA AKIWA ANAENDESHA PIKIPIKI NA PIKIPIKI YAKE KUACHWA

HATARI: AUAWA KWA KWA KUKATWA NA MAPANGA AKIWA ANAENDESHA PIKIPIKI NA PIKIPIKI YAKE KUACHWA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter  Mguluchuma
  Katavi yetu blog
 Mtu mmoja  aliyefahamika  kwa jina la  Heleni Malembeka (40) Mkazi wa  Kijiji cha Ikuba Tarafa ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele  Mkoani Katavi  ameuawa  kwa  kukatwa katwa na mapanga  kichwani na shingoni wakati akiwa anaendesha pikipiki.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari  aliwaambia waandishi wa Habari jana kuwa tukio hilo lilitokea hapo juzi  wakati wa  mida ya saa tatu na nusu katika Kitongoji cha Usumbura Kijiji cha Ikuba.
 Alisema siku hiyo ya tukio  marehemu  alikuwa  akiendsha  pikipiki  aina ya Toyo  yenye rangi  nyekundu  isiyokuwa na namba za  usajiri .
 Marehemu huyo alikuwa akitokea Kijiji cha Usevya Tarafa ya Mpimbwe  akiwa anaelekea nyumbani  kwake katika Kitongoji cha Usumbura ndipo  akiwa njiani  alivamiwa na watu wasiojulikana  na kufanyiwa  mauwaji  hayo.
Kamanda Kidavashari alisema  wauaji hao  baada ya kufanya mauaji walitokomea kusiko  julikana  na kuiacha pikipiki hiyo ya marehemu  Heleni Malembeka bila kuichukua.
Alisema mpaka sasa chanzo cha  mauaji hayo  bado hakijafahamika  na upelelezi wa tukio hilo  unaendelea  kwa polisi   wakiwa wanashirikiana  na wakazi  wa eneo la Kijiji cha Ikuba  ili kubaini  sababu  zilizosababisha mauaji  hayo.
Kidavashari aliwaambia waandishi wa Habari  kuwa mpaka sasa  hakuna mtu wala watu  walioshukiwa na kukamatwa  kuhusiana  na tukio hilo .
Hilo ni tukio la nne kwa kipindi cha siku nne kutokea kwa mauwaji ya aina hii ya watu kuuawa  katika Mkoa wa Katavi na watu  wanaofanya vitendo hivyo  kuuwa na kutochukua kitu chochote cha marehemu hao .

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa