Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter Mguluchuma
Katavi yetu blog
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima anatarajia kuunda tume ya kuchunguza madai ya wakulima wa Chama cha Msingi cha Tumbaku cha Mpanda kati wanao dai malipo yao ya pili ya mauzo ya Tumbaku .
Mwamlima alitowa kauli hiyo hapo juzi wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari juzi ofisini kwake katika Mtaa wa Ilembo Mjini hapa.
Alisema afisi yake imekuwa ikipokea malalamiko ya wakulima wa Tumbaku wa chama cha Msingi Mpanda Kati juu ya kutolipwa malipo yao ya pili ya mauzo yao ya Tumbaku ya msimu uliopita .
Alitaja malalamiko mengine ya wakulima hao kuwa wanakilalamikia Chama hicho kuwa kinawakata fedha nyingi kwenye mauzo yao ya Tummbaku kwa ajiri ya gharama za upandaji wa miti kiwango ambacho akina uhalisia wa idadi ya miche ya miti wanayokuwa wamepewa kupanda.
Mwamlima alisema Serikari inathamini sana vyama vya msingi hivyo hayuko
tayari kuona Chama hicho cha Msingi cha Mpanda Kati kinakufa au
kinagawanyika kwani lengo la Serikali ni kuona vyama vyenye nguvu.
Alisema zao la Tumbaku linamchango mkubwa sana katika kuchangia mapato ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda.
Alifafanua kuwa tume hiyo ya uchunguzi atakayoiteuwa itaanza kufanya kazi hiyo mapema wiki ijayo na itatokana na watu wa idara mbalimbali na vyombo vya usalama .
Hivi karibuni Mkuu huyo wa Wilaya alimwagiza Afisa ushirika wa Wilaya hiyo kuitisha mkutano mkuu wa dharula kwa ajili ya kujadili madai yao ya malipo ya pili ya mauzo yao ya Tumbaku hata hivyo mkutano huu ulishindwa kumalizika baada ya wakulima wa chama hicho kushindwa kufikia muafaka na viongozi wao.
0 comments:
Post a Comment