Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter
Mguluchuma
Katavi yetu blog
Mkuu wa Wilaya ya
Mpanda Paza Mwamlima amesema kuwa
vyombo vya habari vikitumika vibaya
vinaweza kusababisha kutokea kwa machafuko na mfarakano
Mwamlima alitowa kauli hiyo hapo huzi wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa
Habari juzi ofisini kwake mjini hapa
Alisema
kuwa vyombo vya habari vinaumuhimu
mkubwa sana hivyo ni budi vishirikiane na Serikali kwa kusaidia kuelimisha jamii
Alieleza
vyombo vya habari vikitumiwa
vizuri vinauwezo mkubwa wa kuelimisha jamii kwa haraka
hivyo ipo haja ya kushirikiana
kwa karibu zaidi na Serikali ili kutowa elimu kwa wananchi
Hivyo
endapo vitatumika vibaya upo uwezekano mkubwa wa kusababisha machafuko
na mfarakano kutokana
na watu kuwa na imani kubwa na vyombo vya habari
Alisema
waandishi wa habari wanao wajibu
wa kuandika habari ambazo sio za upande
mmoja kama ambavyo wanavyo fanya baadhi
ya waandishi wa habari kwa kutowa habari
za upande mmoja tuu
Alieleza ni
vizuri waandishi wa habari wakazingatia maadili yao kwa kuandika habari
zenye ukweli kwa kusikiliza pande
zote mbili badala ya kutoa habari za upande mmoja tuu bila
kusikiliza na upande wa pili
0 comments:
Post a Comment