Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter Mguluchuma
Katavi yetu blog
Serikali Wilayani Mpanda
Mkoa wa Katavi imeziondoa kaya
zaidi ya 180 zenye jumla ya watu 596 ambao
walikuwa wakiishi kwenye hifadhi za
mistu na kujenga nyumba ndani ya Hifadhi
ya Taifa ya Katavi
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima aliwaambia Waandishi wa Habari jana ofisini
kwake kuwa zoezi la
kuwahamisha watu hao
lilifanyika kuanzia Desemba
5 hadi Desemba 12
mwaka huu
Alisema katika zoezi hilo waliweza kushuhudia kuwepo kwa uharifu wa kuchungia mifugo , ujangili
watu kujenga nyumba na
kulima katika maeneo tengefu
Kaya 186 zenye
watu 596 wameondolewa kwenye maeneo
hayo ambapo jumla ya vibanda 354
viliharibiwa na kuteketezwa kwa moto
Mwamlima alisema
watuhumiwa 18 walikamatwa kwenye
kwenye zoezi hilo baada ya
kupatikana na makosa mbalimbali
Aliyataja baadhi ya makosa waliokamatwa nayo kuwa ni
kufanya ujangili kufanya shughuli za kilimo kujenga ndani ya hifadhi ya Taifa ya Katavi kuchungia mifugo na
kuvuna magogo ndani ya hifadhi bila kuwa na kibali
Maeneo ya hifadhi
yaliokuwa yamevamiwa na watu hao ni msitu wa hifadhi wa Tongwe, msitu wa hifadhi wa Nkamba
na ushoroba wa wanyama wa Lyamgoroka
Mwamlima alisema kwenye zoezi hilo wamekumbana na baadhi ya changamoto mbalimbali katika utekelezaji wa zoezi hilo na kuzitaja baadhi ya changamoto kuwa ni
Uwepo mgumu wa kuwakamata
wahusika wa jamii ya kifugaji wenye
mifugo na badala yake
wamewakamata watoto wadogo wenye umri
wa miaka sita na kumi kutokana na
wazazi wao kutokuwepo kwenye eneo husika
Changamoto nyingine ni
ufinyu wa bajeti na ushirikiano
mdogo wa baadhi ya viongozi wa Kata na vijiji kutotoa ushirikiano uliostahili
Zoezi hilo liliwashilikisha Idara
za ardhi na maliasili ,polisi ,
Takukuru , usalama wa Taifa na askari
walinzi wa mistu ya vijiji(VGS)
0 comments:
Post a Comment