Home » » CHADEMA KATAVI KWAZUKA VURUGU VIONGOZI WAO WAFUNGIWA MLANGO KWENYE UKUMBI WA MKUTANO WAANDISHI WATIMULIWA

CHADEMA KATAVI KWAZUKA VURUGU VIONGOZI WAO WAFUNGIWA MLANGO KWENYE UKUMBI WA MKUTANO WAANDISHI WATIMULIWA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na  Walter  Mguluchuma
Katavi yetu

Vurugu   kubwa zimeibuka  katika mkutano  wa Chama  cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Katavi   na kusababisha   kundi la wafuasi  wa chama  kuwafungia  mlango viongozi wao wa Kanda , Mkoa  na Wilaya  wasitoke  nje ya ukumbi wa mkutano baada ya kutangaza kuharishwa kwa mkutano huo kutokana na vuurugu za wafuasi hao waliokuwa wakishinikiza baadhi ya viongozi wao wa ngazi ya Mkoa  na Wilaya wajiuzuru 

Vurugu  hizo zilitokea  hapo jana   kwenye ukumbi wa Katavi Resort ulioko Mjini  hapa  majira ya saa  saba  mchana  licha  ya ukumbi huo  kuwa umezungukwa  na ulinzi wa askari wa jeshi la polisi ambao walikuwa wapata taarifa kabla ya kuanza kwa mkutano huo  kuwepo kwa dalili za  vurugu 

Wafuasi hao  na wanachama wa  Chadema  wakiwemo waliokuwa wagombea  wa udiwani  wa Kata  mbalimbali  walianza kutowa maneno  ya kuwashutumu  viongozi wao   mara baada ya kufunguliwa  kwa mkutano huo  na   mratibu wa  Chadema  wa Kanda ya  Magharibi Cristophar Namwanji 

Mara  baada ya kufunguliwa kwa mkutano huo  mmoja   wa wafuasi hao   Shukuru alisimama na  kueleza kuwa yeye na   wenzake  hawana imani  na  viongozi wao  kwa kuwa ni wasaliti 

 Kauli hiyo ambayo iliungwa mkono na kundi kubwa ndani ya mkutano huo huku wakiwa  wanapaza sauti  na kusema kuwa viongozi  hao waliwasaliti wakati wa  uchaguzi mkuu na kusababisha  wasipate  jimbo hata moja wakati wa uchaguzi mkuu  kati ya majimbo matano yalioko Mkoani  Katavi 

Mratibu  wao wa Kanda ya Magharibi   Namwanji  alijaribu  kuwasihi wafuasi hao   wawe watulivu  lakini  ilishindikana  hari ambayo ilimfanya Mwenyekiti wao  Kanda ya Magharibu Mussa   Masanja atoke nje ya ukumbi  na kufanya  mashauriano na Mkuu wa  Kituo cha Polisi cha Mpanda Mjini  ambapo walishauliana kuwa mkutano huo uharishwe kutoka na  hari ya vurugu

Masanja baada ya kuingia  ndani  aliwasilisha  wazo la kuharishwa kwa mkutano huo kwa viongozi wenzake wa Kanda na mkoa ambao  wote kwa pamoja  walikubaliana kuharishwa kwa mkutano huo  na  walimtaka   mratibu wao  hawafahamishe wajumbe wa mkutano  huo kuharishwa kwa mkutano 

 Baada ya  mratibu wao wa Kanda kutangaza  kuharishwa kwa mkutano huo kundi la   wajumbe wa mkutano huo  lilianza kupiga kelele kuwa haiwezekani  na kuwaamuru  viongozi wao wasitoke nje  mpaka  hapo watakapo kuwa wamejiuzuru  viongozi wanao watuhumu kusaliti  chama chao 

Vurugu  zilanza  ndani ya ukumbi huo wa Katavi Resort  huku   milango ikiwa imefungwa kwa lengo la kuhakikisha  viongozi wao   hawatoki nje ya ukumbi huo na wao  baada ya kuona  hari ya usalama wao uko hatarini  waliamua  kufuata matakwa ya wafuasi hao ya kuendelea  na mkutano huo 

 Hata  hivyo    kabla ya kuendelea  kwa mkutano huo Mwenyekiti wa Chadema wa Mkoa wa Katavi Laulent  Mangweshi alisimama na kuwataka  waandishi wa  Habari wote waliomo  ndani ya ukumbi huo watoke nje  hari ambayo ilipelekea  wajumbe wa mkutano huo   kuwanza kupiga moyowe ya kusema  msiondoke msiondoke tunawahitaji muwemo huo hata hivyo waandishi waliomua kutoka nje

 Hivi   karibuni   vurugu  ziliibuka  katika  ofisi  za Chadema  Mkoa wa Katavi  baada ya kundi la wafuasi wa Chama hicho na kuwashinikiza  viongozi wao wajiuzuru  kwa kuwa waliwasaliti  wakati wa uchaguzi  mkuu uliopita

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa