Home » » HOT: YEYOTE ATAKAEUGUA KIPINDUPINDU KUSHTAKIWA -DC

HOT: YEYOTE ATAKAEUGUA KIPINDUPINDU KUSHTAKIWA -DC

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter  Mguluchuma
Katavi yetu blog
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza  Mwamlima  ameagiza kuwa  mtu yoyote atakae ugua  ugonjwa wa kipindupindu  akitibiwa na kupona  atakamatwa na kushitakiwa  kwa kosa la kukiuka taratibu za afya
Mwamlima alitowa  agizo hilo hapo  jana wakati wa uzinduzi wa usafi wa wa  mazingira  na upandaji wa miti  uliofanyika  katika   eneo la stendi kuu ya mabasi yaendayo  Mikoani  katika Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi
 Alisema   mtu yoyote atakae ugua  ugonjwa wa kipindupindu  katika  Wilaya  ya Mpanda atahakikisha  anapatiwa huduma ya matibabu  na baada ya kutibiwa na kupona  atakamatwa na kufunguliwa  mashitaka ya kukiuka  taratibu za afya
 Mwamlima  alieleza kuwa  ugonjwa wa kipindupindu  unasababishwa na uchafu  hivyo  bila kuwa   na  mazingira ya uchafu  mtu hawezi kuugua ugonjwa huo
 Alisema  ni wajibu wa  kila mtu  kuishi  kwenye  mazingira ya usafi  na wanatakiwa kupenda usafi  na kuuchukia  uchafu  ndio itakuwa  njia pekee ya  kuepuka  magonjwa ya mlipuko
 Alifafanua kuwa  jambo la usafi  sio geni  kwani kila  mtu  anatambua maana ya  usafi  hivyo ni  vizuri kila  mtu  atambua  umuhimu wa usafi
 Pia  Mkuu huyo wa Wilaya  amepiga marufuku  baa zisifunguliwe  muda  wa kazi wala watu kucheza  bao  na watu kushinda  kwenye vijiwe vya vinavyouza  kahawa
Kwa upande  Mkuu wa  Mkoa wa Katavi Dr    Ibrahimu  Msengi  amewaagiza wananchi  wa Manispaa  kuhakikisha maeneo yao ya kuishi na wanayofanyia shughuli za biashara yanakuwa katika hali ya usafi
 Alisema   kila jumamosi  wananchi wa Manispaa hiyo  waakikishe  siku hiyo wanaitumia kwa ajiri ya kufanya usafi kwenye mitaa yao na siku ya jumamosi ya kwanza ya mwezi itakuwa inatumika kwa ajiri ya manispaa nzima ya Mpanda
Pia  aliitaka  Manispaa hiyo kutumia  sheria ndogo ndogo za Manispaa hiyo kuwachukulia hatua watu wote ambao  waeneo  yao yatabainika kuwa na uchafu
Nae  Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Hamis Mkele  alieleza kuwa   uzinduzi huo  wanautumia  kama sehemu ya kujitathimini  katika   maswala   mazima ya  usafi wa mazingira
 Alisema  Halmashauri hiyo  ilianzishwa   mwaka 2007  kama  Halmashauri ya Mji  na   Julai  mwaka huu imepandishwa hadhi kuwa Manispaa  hivyo  wameona wanalo jukumu  sasa la kujipanga kwenye maswala ya usafi wa mazingira kama Manispaa na sio kama Halmashauri ya Mji

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa