Home » » KATAVI WASHAURI KUTII MAELEKEZO YA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

KATAVI WASHAURI KUTII MAELEKEZO YA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter Mguluchuma
Katavi
Wakazi wa Mkoa wa Katavi wametakiwa  kutii maelekezo yanayotolewa na Tume ya Taifa ya uchaguzi  ili  wasivilazimishe vyombo vya ulinzi na usalama  vitumie nguvu pasipo kuwa na sababu
Wito huo umetolewa hapo jana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Mwandisi Emanuel Kalobelo wakati wa kikao cha wadau  wa amani kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda
 Alisema endapo wananchi wa Mkoa wa Katavi watatii maelekezo yanayotolewa na  Tume ya Taifa ya uchaguzi kwa ajiri ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 kutakuwa na uwezekano wa kufanya kwa  uchaguzi wenye amani 
Mwandisi Kalobelo aliwaeleza wajumbe wakikao  hicho kuwa endapo  wananchi haatatii maelekezo yanayotolewa na tume ya Taifa ya uchaguzi kutakuwa na kila dalili za uvunjikaji wa amani na matokeo yake  wananchi watakuwa  wamevilazimisha vyombo vya ulinzi na usalama  kutumia nguvu pasipo  sababu yoyote
Nae Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri  Kidavashari alieleza kuwa Tume ya uchaguzi  imeisha towa maelekezo ya kuwataka wananchi  wasikae  karibu na vituo vya kupigia kura  na badala yake wakipiga kura warudi makwao au kwenye biashara zao licha ya kanuni ya uchaguzi kuruhusu watu wakae umbali wa mita 200 kutoka eneo la kituo cha kupigia kura
Alisema kuwa sheria Namba  73 inawapa mamlaka jeshi la Polisi kuzuia mikusanyiko ya makundi ya watu  ambao wanaweza  kusababisha uvunjikaji wa amani
Kwaupande wake Vicenti Nkana alisema kuwa   kila mzazi Mkoani Katavi anao wajibu  wa kuwaonya  watoto  kutofanya siku ya uchaguzi wa Oktoba 25 yale ambayo yamekazwa na Tume ya Taifa ya uchaguzi
 Alisema  kama  viongozi wa vyama vya  siasa watajitambua   kuwa wapo kwa ajiri  ya manufaa ya Taifa  wakijitambua hivyo uchaguzi mkuu utakuwa wa amani na utulivu
Katika kikao hichoviongozi wa vyama vya upinzani  walikuwa wakitetea kuwa  watu waruhusiwe  kukaa umbali wa mita 200 kutoka kwenye vituo vya kupigia kura kama ambavyo  kanuni yatume ya uchaguzi inavyoeleza  hata hivyo wajumbe wengi wa kikao hicho walipinga hoja  hiyo kwa kile walichodai kuwa wakiruhusiwa kukaa umbali huo upo uwezekano wa kutokea kwa uvunjikaji wa amani
Kikao hicho  chenye lengo la kujadili hari ya usalama na amani wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi kiliwashirikisha  wajumbe wa  kamati za ulinzi na usalama wa Wilaya zote za Mkoa wa Katavi ,wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa Mkoa wa Katavi  viongozi wa tume ya Taifa ya uchaguzi, viongozi wa madhehebu ya Dini wazee maarufu na Waandishi wa Habari

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa