Home » » HOT NEWS: 3,870 AMBAO SIO RAIA WA TANZANIA WABAINIKA KUJIANDIKISHA KATIKA DAFTARI LA WAPIGA KURA .

HOT NEWS: 3,870 AMBAO SIO RAIA WA TANZANIA WABAINIKA KUJIANDIKISHA KATIKA DAFTARI LA WAPIGA KURA .

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
N a  Walter  Mguluchuma
Katavi 
Jumla ya watu  3,870  walioandikishwa kupiga kura  kwa ajiri ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 wamebainika  wakiwa sio Raia wa Tanzania  na vitambulisho vyao vimerejeshwa kwa   Tume  na wameondolewa  kwenye  Daftari la wapiga kura
Hayo  yalisemwa  hapo  jana  na  Afisa wa  wa tume ya uchaguzi wa Kanda  ya  nyanda za juu   Jane  Tungu  kwenye hutuba  yake ya ufunguzi wa  mkutano  wa tume  na viongozi wa vyama vya siasa    wa Mkoa wa Katavi uliofanyika  katika  ukumbi wa Chuo Kikuu huria cha Mkoa wa Katavi
Alisema  baada ya  kuchakata  Daftari  mchakato wa mwisho  wa kuhakiki Daftari  hatimae  idadi  halisi ya  wapiga kura  katika daftari  la kudumu  la wapiga kura  idadi yao ni  watu 23,154,485  ambapo  waliojiandikishwa  na Tume  na Tume  ya Taifa ya  uchaguzi (NEC)  na  503,193 waliandikishwa na Tume  ya uchaguzi  Zanzibar(ZEC)
 Hata hivyo  baada ya  ya kuhakiki  na  uchakataji  wa taarifa  za wapiga kura  Tume  ilibaini  kuwa jumla  ya  wananchi  231,955 waliandikishwa zaidi ya mara moja  na 3,870 walikuwa sio Raia wa Tanzania
 Alisema Tume  imejipanga  kuhakikisha  kila mpiga kura  mwenye sifa  za kupiga kura  anapiga kura yake siku hiyo ya uchaguzi  pasipo  kubughudhiwa
 Jane aliwaasa  viongozi hao wa vyama vya siasa  wazingatie  sheria  na taratibu  za uendeshaji  wa tatatibu za uchaguzi  na waepuke  kutowa lugha  zozote  za uchochezi  zinazo weza  kuleta  uvunjifu wa  amani  na kuhatarisha  maisha ya Watanzania
Alifafanua  kwamba uzoefu  unaonyesha  kwamba  katika kampeni zinaendelea  pale ambapo  wafuasi  wa vyama tofauti  wanapokutana  uwezekano wa kutokea  vurugu ni mkubwa  na   sehemu nyingine  vurugu zimetokea  na kusababisha maafa,majeruhi  na uharibifu wa mali
Hivyo  endapo  kila  chama  kitaamua  kuwaelekeza  wafuasi  wake  kubaki  kwenye vituo vya  kupigia kura  upo uwezekano  mkubwa  wa kutokea  vurugu  ambazo  zinaweza  kupelekea  kuwatia  hofu  na   kuwasumbua wapiga kura  ni mkubwa  hivyo kuhujumu  zoezi  la  upigaji kura

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa