Home » » MWANDISHI WA HABARI AONGOZA KURA ZA MAONI ZA KUGOMBEA UBUNGE

MWANDISHI WA HABARI AONGOZA KURA ZA MAONI ZA KUGOMBEA UBUNGE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
Mwandishi wa  habari    wa  gazeti  la   The gudian  Gerald  Kitabu  amewashinda wagombea  wenzake  watatu  kwenye  kura za  maoni  za kuomba   kuteuliwa  kugombea  Ubunge wa  Jimbo la  Nsimbo  kupitia  chama  cha  CHADEMA
Kitabu   aliwashinda    wagombea  wengine  watatu  katika   kura za  maoni   za kugombea  Ubunge wa  Jimbo  la  Nsimbo  zilizofanyika  jana   katika    ukumbi  wa  Songambele    Wilaya ya  Mlele  Mkoani  hapa
Katika  uchaguzi huu wa kura za  maoni  za  jimbo  hilo  jumla ya  wanachama  wanne wa  wachama  hicho  walijitokeza  kugombea  nafasi ya  kuomba  kuteuliwa  na  chama  hicho  kugombea  ubunge kwenye  uchaguzi mkuu wa  oktoba  25  mwaka huu
 Wanachama  hao wengine  waliogombea  nafasi  hiyo    ya kuomba kuteuliwa kugombea  ubunge wa  jimbo la  Nsimbo  ni Mpate  Samwel  Sullemani, Kayagambe  Jaston  Wilson na Busagala   Mwandu   Godoka
Gerald  Kitabu  katika  uchaguzi  huo wa kura za  maoni   alipata  kura  65  Mpate  Sullemani  kura  37,Kayagambe   Wilisoni   kura    36 na   Mwandu   Godoka  alipata  kura   tisa
Katika  uchaguzi  mkuu wa Oktoba  25  Gerald  Kitabu  kuenda  akapambana  na   mgombea  mmoja kutoka  CCM  ambapo jula ya wana CCM  sita  wamechukua  fomu  za kuomba kuteuliwa  kugombea  jimbo  hilo
Wanachama  hao  ni  Said   Amour  Arfi  ,Richald  Mbogo ,Hassanal   Shabir(Dalla),Manamba  Emanuel  na  Frenk     Mapesa
 Katika  uchaguzi  mwingine  mwinge wa kura za  maoni  za kumpata   mgombea  ubunge wa  Jimbo  jipya la  Katavu(CHADEMA)  uliofanyika  jana    huko  Tarafa ya  Mpimbwe  Wilaya Laulenti  Magweshi  ameweza kuwashinda wagombea   wenzake  sita  wa   Chama  hicho

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa