Home » » CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI KATAVI CHA PATA VIONGOZI

CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI KATAVI CHA PATA VIONGOZI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
Chama  cha Waandishi wa  habari cha Mkoa wa Katavi(KPC) kimewachagua  viongozi watako  kiongoza  chama  hicho  kwa kipindi  cha miaka  mitatu  ijayo
 Viongozi  hao  walichaguliwa  hapo  jana    na   kwenye  mkutano  mkuu wa  uchaguzi  wa  chama  cha   waandishi wa  habari wa   Mkoa wa  Katavi  uliofanyika  kwenye  ukumbi wa   Parokea  ya  Kanisa  Katoliki  jimbo  la  Mpanda
 Uchaguzi huu  ambao ulivutia hisia  za watu  wengi wa  Mkoa  wa  Katavi ulisimamiwa  na  mjumbe  wa  wa  bodi ya muungano  wa  kilabu za  waandishi wa  habari   hapa   nchini (UTPC)  Deo  Nsokolo  ambae  pia ni mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa  habari wa Mkoa wa Kigoma
Katika  uchaguzi huu  wajumbe wa mkutano mkuu  walimchagua  walter Mguluchuma kuwa  Mwenyekiti wa  Chama  hicho  baada ya kuwa  mgombea  pekee wa nafasi hiyo na kupigiwa kura zote za ndio
Makamu  Mwnyekiti  alichaguliwa  Elias  Milwano  ambae  alikuwa  mgombea pekee wanafasi  baada  ya kupa  kura  10  kati ya kura 11  ambapo  kura moja iliharibika
Katibu  Mkuu alichaguliwa   Pascal  Katona  na  katibu  msaidizi  alichaguliwa  Arine  Temu  baada ya kushinda  wandishi wa  habari wa TBC Adolfu   Mbata  kwa kura  saba kwa nne na mtunza  mwasibu wa  klabu  alichaguliwa  Frida  Ngozi
Mara  baada ya kutangaza  matokea  hayo  msimamizi  wa  uchaguzi huo  Deo  Nsokolo aliwataka  viongozi  waliochaguliwa   kuiongoza  klabu  hiyo kwa kufuata misingi ya katiba
 Alisema wapo baadhi ya viongozi wamekuwa wakiongoza klabu hizo  kama mali zao binafsi na matokeo yake ndio imekuwa ndio  vyanzo vya migogoro hivyo ni  vizuri wakaongoza kwa misingi ya uwazi
 Pia  amewataka  kuwashirikisha wanachama  wa klabu  hiyo kwenye  maswala yote ya mali za  chama  hicho ili   pasipo  kuwaficha  jambo lolote linalohusiana  na mali za klabu

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa