Home » » WANANCHI WASIMAMISHA MSAFARA WA NAIBU WA ARDHIWAKIDAI FIDIA YA ARDHI YAO

WANANCHI WASIMAMISHA MSAFARA WA NAIBU WA ARDHIWAKIDAI FIDIA YA ARDHI YAO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
Baadhi ya Wananchi wa Mtaa wa Kazima  Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi juzi katika hari isiyotarajiwa waliusimamisha  msafara wa  Naibu Waziri wa  Ardhi  Nyumba  na maeneleo ya makazi   Angellah  Kairuki  wakitaka  kufahamu  hatima ya fidia yao ya  ardhi yao   ekari  500 zilichukuliwa na Halmshauri ya Mji wa Mpanda kwa ajiri ya ujenzi wa chuo kikuu cha kilimo
 Tukio hilo  la kusimamishwa kwa msafara huu wa Naibu  Waziri lilitokea hapo juzi majira ya saa tano asubuhi  katika  eneo la mtaa wa Ilembo umbali wa kilometa tano kutoka Mpanda Mjini
 Wananchi hao wa  Mtaa wa  kazima wanaidai Halmashauri  ya Mji wa Mpanda kiasi cha shilingi milioni mia  nane  kama fidia ya adhi yao iliyochukuliwa na Halmashauri ya Mji wa Mpanda  toka  mwaka 2011   kwa ajiri ya kupisha ujenzi wa   chuo kikuu cha kilimo huko  katika eneo la Kazima  mjini Mpanda
 Katika  tukio  hilo  wananchi hao walikuwa  wamejipanga pembeni ya barabara  wakiwa wanausubiri msafara wa Naibu  Waziri  Kairuki  uliokuwa  umetokea kwenye  Ofisi ya Mkuu wa Mkoa  zilizopo kwenye mtaa wa   Ilembo ambako  alikuwa na kikao na viongozi wa Mkoa wa Katavi ambao walikuwa wakimpatia  taarifa ya migogoro ya adhi ilipo katika Mkoa wa Katavi
Mara baada ya kumaliza kikao chake na  viongozi wa Mkoa  msafara huo ulianza  safari ya kuelekea  mjini Mpanda  ndipo baada ya muda mfupi baada ya kuanza msafara huo  wananchi hao walisimamisha msafara huu hari ambayo ilimlazima   Naibu  Waziri  aweze  kusimama
Baada ya kusimama   Naibu  Waziri  Kairuki alishuka kwenye gari  lake na kisha alisikiliza  kero yao na  aliwaahidi kurudi tena Mkoani  Katavi  hapo mwezi  Agosti na ndipo atakuwa na muda mzuri zaidi wakuongea na  Wananchi hao  hari ambayo  iliwafanya  wananchi hao walidhike na kauli hiyo na kisha msafara huu uliendelea
 Awali  kabla ya tukio hilo   katika kikao kilichofanyika  katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi  baina ya waziri  Kairuki na viongozi wa Mkoa wa Katavi  alisema kuwa  madai ya fidia ya ardhi kwa wananchi wa hao  yamekuwa ni ya muda mrefu  hivyo wananchi hao  wanatakiwa walipwe fidia yao mapema
 Alisema  wananchi hao waliwahi  kufika mpaka ofisini kwake  Mjini  Dodoma na kumfikishia malalamiko hayo ya kuchelewa  kulipwa   fidia yao ya shilingi milioni  mia nane
  Aliziagiza Halmashauri zote hapa  Nchini  kutenga fedha za  kuwalipa wananchi fidia  ya adhi  kabla ya kuchukua kwanza adhi wa wananchi wanapaswa wawe wanalipwa kwanza na pia itasaidia kupunguza kero kwa wananchi kudai fidia zao
Mkurugenzi wa Halmashauri ya  Mji wa Mpanda  alimuhakikishia  Naibu Waziri kuwa swala la wananchi hao  analishughulikia kwani hata yeye alilikuta  toka miaka miwili iliyopita  alipo  hamishiwa kwenye  Halmashauri hiyo
Hata hivyo  Lukanga alipoulizwa kama hati ya kiwanja hicho Halmashauri inayo alijibu kuwa Halmashauri inayo kopi ya hati ya kiwanja hicho  na alipotakiwa aeleze hati yenye ipo wapi  katika hari ya kushangaza alijibu kuwa hati hiyo imewekwa   Bank na ilipekwa na baadhi wajumbe wa bodi waliokuwepo
 Baada ya majibu  hayo Naibu Waziri aliagiza hati hiyo ifatiliwe huko iliko  wekwa  Bank  wa kuwa  haiku  pelekwa bank wa kufuata utaratibu  na upo uwezekana hati hiyo ikatumiwa na watu kwa manufaa yao binafsi

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa