Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter Mguluchuma
Katavi
Waziri wa mambo ya
Nchi za nje wa Tanzania
Benard Membe anayeomba
ridhaa ya kuteuliwa kugombea
Urais na Chama
cha Mapinduzi (CCM) anasema
mgombea yoyote wa nafasi hiyo aliyeomba ridhaa ya kuteuliwa akishindwa
kushinda kwenye Halmashauri kuu
ya Taifa au kwenye Mkutano mkuu asipo kubali matokeo yakushindwa mtu huyo anamfananisha na Kenge
Membe alitowa
hiyo mjini Mpanda hapo jana
nje ofisi za CCM
Wilaya ya Mpanda
mara wakati alipokuwa
akiwahutubia wanachama wa CCM na
Wananchi wa Mji wa Mpanda mara baada ya kudhaminiwa na wanachama
225 fomu za kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwa mgombea urais kupitia
CCM
Alisema chama cha mapinduzi kimekuwa na utaratibu wa
wagombea wake wanao wania Urais
kukubali matokeo pindi wanapo kuwa wameshindwa hivyo hata wa waliomba ridhaa mwaka huu ya
kuomba kuteuliwa na CCM atakae shindwa anapaswa akubali matokea mgombea ambae atashindwa kwenye kura kwenye wa NEC na kwenye mkutano Mkuu wa CCM akipinga matokeo hayo yeye Membe anamfananisha
mtu huyo sawa na Kenge
Alieleza CCM
haijawahi kufanya makosa kwenye uteuzi wake wa mgombea Urais
hivyo kwa kwa mgombea atakae shindwa
lazima akubali matokeo
alirudia tena kauli yake anae pinga ni sawa na Kenge
Alisema katika
wagombea wote waliomba ridhaa ya
kuteuliwa na CCM kugombea
Urais yeye mtu anae muogopa kushindana nae ni Mizengo Pinda peke yake ambae ni Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri
ya Muunganano
Membe alieleza
endapo Pinda angekuwa hayumo
katika watu waliomba ridhaa ya
kuteuliwa kupitia CCM basi moja kwa moja angekuwa yeye Membe ndiye
angekuwa mshindi na moja kwa moja
angekuwa na uhakika wa kuteuliwa na chama chake kuwa mgombea Urais kupitia CCM
katika uchaguzi mkuu wa mwezi oktoba
mwaka huu
Alisema katika wagombea wote waliomba ridhaa ya
kuteuliwa na CCM kugombea Urais hakuna
mgombea aliye na sifa kama yeye
kwani hakuna mgombea ambae anae
yajua mambo ya nchi za nje kama yeye na mambo ya ndani ya nchi kama
Membe
Waziri Bebard
Membe amepata jumla ya wanachama
wa CCM 225 waliomdhamini kwenye fomu za
kuomba ridhaa kuteuliwa kugombea urais kupitia CCM baada ya kumaliza shuguli
hiyo Waziri Membe alielekea Mkoani Rukwa
kuendelea na zoezi la kutafuta wadhamini
0 comments:
Post a Comment