Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limekamilisha ujenzi wa mradi
wa nyumba 70 zilizopo
katika eneo la Ilembo Wilayani Mpanda Mkoa wa Katavi zilizogharimu zaidi ya shilingi bilioni mbili
Hayo yalisemwa hapo jana na Meneja wa shirika la
Nyumba la Taifa wa Mikoa ya
Katavi na Rukwa Neemia Msigwa wakati alipokuwa akitowa taarifa ya ujenzi wa nyumba ya shirika iliyojengwa na
inayoendelea kujengwa katika Mikoa ya
Katavi na Rukwa mbele ya Naibu Waziri wa Ardhi
Nyumba na maendeleo ya
Makazi Angellah Kairuki wakati wa ziara yake ya kukagua
miradi ya ujenzi wa nyumba za shirika
hilo Mkoani Katavi
Alisema
mradi wa ujenzi wa nyumba sabini
za makazi zilizopo katika eneo la mtaa wa Ilembo kilimeta tano kutoka Mpanda mjini ambao kwa sasa umekamilika ulianza
kujengwa Desemba 2012 ambao kwa sasa umekamilika mradi huo umegharimu kiasi cha
Tsh Bilioni 2.1
Msigwa alieleza nyumba
hizo 70 tayari NHC imepata
mnunuzi wa kuzinunua ambao ni
Halmashauri ya Mji wa Mpanda
ambao wako kwenye mchakato wa kupata fedha za mkopo za kununulia nyumba hizo kwenye mabenki rafiki
Alifafanua kwa
upande wa Mikoa ya Katavi na Rukwa shirika
la NHC lina jumla ya miradi minne
ambapo miradi mitatu ipo katika Mkoa wa Katavi na mradi mmoja
upo katika Mkoa wa Rukwa
Aliitaja miradi hiyo kuwa ni
mradi wa jengo la kitega
uchumi Paradise uliopo
mjini Mpanda mradi wa
nyumba 20 za makazi
za gharama nafuu Inyonga uliopo
Halmashauri ya Wilaya ya
Mlele Mkoani hapa na mradi
wa nyumba za makazi za
gharama ya kati jangwani
Town House ulipo manispaa ya
Sumbawanga Rukwa
Alisema mradi wa jengo la kitega uchumi la Paradise
wa ghorofa nne utakaogharimu kiasi chashilingi bilioni 3.1 unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba
mwaka huu mradi wa Inyonga unatarajia
kutumia kiasi cha shilingi bilioni 1.2 na utakamilika mwishoni mwa mwaka huu
na mradi wa jangwani Sumbawanga wa
ghorofa moja nao utakamilika
mwishoni mwa mwaka huu
Kwa upande
wake Mkurugenzi wa
utawala na uendeshaji wa Mikoa wa NHC Raymond Ndolwa alieleza kuwa shirika hilo linatarajia kuanza ujenzi wa nyumba za gharama nafuu na ndogo zaidi
kuliko wanazo jenga sasa
Alisema lengo la
shirika hilo kujenga nyumba kwenye mikoa mbalimbali ni kusogeza maendelea karibu zaidi na wananchi
Naibu Waziri
wa Ardhi
nyumba na Maendeleo ya
Makazi Angellah Kairuki alieleza kuwa
mpaka sasa bado mahitaji ya nyumba za
kuishi ni chache hapa nchini kwa ajiri ya makazi ya kuishi watumishi
Alisema hadi sasa
kuna upungufu wa nyumba milioni moja za kuishi watumishi hapa nchini
na mahitaji ya nyumba yatazidi
kuongezeka siku hadi siku
Aidha
alitowa wito kwa Halmashauri zote
hapa nchini ziendelee kutowa viwanja
kwa NHC ili shirika hilo liendelee kujenga nyumba nyingi za kutosha kwenye maeneo mbalimbali
Naibu Waziri pia alilita shirika la nyumba la Taifa
kuhakikisha linaongeza kasi ya ujenzi wa
wa miradi yake ya nyumba ili iweze kumalizika kwa wakati ili kupunguza
tatizo la uhaba wa nyumba za makazi
0 comments:
Post a Comment