Home » » WAKULIMA WA TUMBAKU KATAVI KUZALISHA TUMBAKU ZAIDI YA KILO MILIONI 14

WAKULIMA WA TUMBAKU KATAVI KUZALISHA TUMBAKU ZAIDI YA KILO MILIONI 14

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
Wakulima wa  zao la Tumbaku  wa Mkoa wa Katavi kupitia  vyama vyao  vya ushirika  vya msingi  wanatarajia  kuzalisha  na kuuza   zaidi  ya kilo  milioni 14 ambazo ni sawa na  zaidi ya tani elfu kumi na nne  kwa msimu wa mwaka 2014 na 2015
 Haya yalielezwa  hapo jana na  wakulima wa Tumbaku wa Mkoa wa Katavi kwenye risala yao iliyosomwa  na Selemani Kaitila kwa niaba ya mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika wa wakulima wa Tumbaku wa Mkoa wa Katavi(LATCU LTD)  wakati wa ufunguzi wa ununuzi wa zao la Tumbaku kwa msimu wa mwaka 2014 na 2015 uliofanyika kwenye chama cha ushirika cha msingi mbele ya mgeni Rasmi mkuu wa Mkoa wa Katavi Dr Ibrahimu Msengi
 Kaitila alisema kuwa  msimu wa kilimo  wa mwaka 2014 na 2015 wakulima  wa vyama vya ushirika vya msingi  wanatarajia kuzalisha na kuuza  tumbaku yenye  jumla ya kilo 14,187,690 ambazo ni sawa na  tani  14,187.61 zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 48
 Msimu wa mwaka uliopita  wakulima wa tumbaku wa Mkoa wa Katavi wanachama  wa  LATCU  walizalisha kilo 13,305,706  za Tumbaku  ambazo ni sawa na tani  13,305.71 zenye thamani ya dola za Kimarekani  dola 30,337,009.68 wastani wa  bei kwa kilo  moja iliuzwa kwa  wastini wa dola 2.28
 Na  Halmashauri za Mkoa wa Katavi  zilipata ushuru wa  uliotokana na Tumbaku  kwa msimu huo  kiasi cha shilingi  Bilioni  mbili  mia  nne  na ishirini na mbili  milioni  laki tisa  na kumi na mbili  na kumi na mbili  elfu
 Alisema zao la tumbaku limekuwa likiendeshwa  kwa mkataba  kati ya wanunuzi   na wakulima wa Tumbaku kwa Mkoa wa Katavi  makampuni yanayo nunua Tumbaku ni mawili ambayo ni  Premium Active(T)  na Tanzania  Leaf Tobacco  company(TLTC)
Alifafanua  jambo kubwa wanalojivunia wakulima wa Tumbaku wa Mkoa wa Katavi  katika biashara  ya Tumbaku  ni kuweza  kulipa  madeni  ya pembejeo kwa asilimia mia moja
Msoma risala   alieleza   kuwa katika kuhakikisha  kilimo cha  Tumbaku  kinakuwa endelevu  katika Mkoa wa Katavi  suala  la utunzaji wa mazingira  kwa kupanda miti  linapewa  uzito  na umuhimu wa pekee
 Alitaja  baadhi ya changamoto  walionayo wakulima wa Tumbaku  ni utunzaji wa  miti  iliyopandwa  imekuwa ikiathiriwa na  uchomaji  holela wa moto  na uchungaji holela wa mifugo
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Katavi  DR  Ibrahimu  Msengi ambae alifungua msimu wa ununuzi wa zao la Tumbaku alisema kuwa vyama vingi vya ushirika  vya msingi vimekuwa na migogoro kutoka na viongozi wanaoviongoza vyama hivyo kutokuwa waaminifu
Alisema  wakulima wa Tumbaku wanatakiwa kuwacha kuwachagua viongozi wanao waongoza kwenye vyama vyao vya msingi  wale ambao  wanajali masilahi ya wakulima na wale wenye  upeo mkubwa ambao wanauwezo wa kuwatetea wakulima  kwenye masilahi yao
Chama kikuu cha ushirika cha  wakulima wa Tumbaku   cha Mkoa wa Katavi LATCU  kinanawachama saba   wa ushirika vya msingi  ambavyo ni  Nsimbo, ukonongo, Katumba. Mishamo  Tamcos, Kasokola,Amcos, Mpanda kati na Ilunde

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa