Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Mkuu wa Wilaya ya
Mpanda Paza Mwamlima awewataka Boda boda
walioko katika Halmashauri ya Mji wa Mpanda Mkoa wa Katavi wachangamkie kujiunga na mfuko wa Bima ya afya NHIF ili waze kupata tiba ya uhakika
Mwamlima alitowa kauli hiyo hapo jana wakati akiwahutubia
wananchi wa Kata ya Mwamkulu wakati wa ziara yake ya kuwahamasisha wananchi wa Halmashauri ya Mji wa Mpanda wajiunge na mfuko wa NHIF
katika ziara hiyo ambayo alikuwa amefuatana na viongozi wa mfuko wa bima ya
afya wa Mkoa wa Katavi na Rukwa wakikuwa wameongozwa na meneja wa mfuko huu wa
mikoa ya Rukwa na Katavi Abdiel Mkayo
Alisema
boda boda wamekuwa wakipata ajari mara kwa mara hivyo wakijiunga na mfuko huo watakuwa na uhakika
wa kupata matibabu pindi wanakuwa wamapata ajari
Alisema sio muda wote huwa wanakuwa na pesa za matibabu hivyo endapo
watakuwa wamejuimga na mfuko
itakuwa kwao ni rahisi kupatiwa
huduma ya matibabu hata kama wanakupokuwa
hawana fedha
Kwa upande
wake Meneja wa mfuko wa bima ya afya NHIF wa mikoa ya Rukwa
na Katavi Abdiel Mkayo alisema kuwa
mfuko huo ni muhimu sana kwa watu ambao wanakuwa wamejiunga na mfuko
kwani sio wakati wote mtu anaweza kuwa
na pesa
Alisema
wako baadhi ya watu wamekuwa na hofu ya kujiunga na mfuko huu kutokana
na kukosekana kwa dawa kwenye vituo vya kutolea huduma
Alifafanu
ukosefu huo wa dawa umekuwa ukichangiwa na ukosefu wa fedha na kamati zinazokuwa zimechaguliwa
kutosimamia ipasavyo vituo vyao vya
kutolea huduma
Nae mratibu
wa mfuko wa afya ya jamii Lesipita
Kalugendo aliwaeleza kuwa
Halmashauri ya mji wa Mpanda imeisha jipanga ili kuhakikisha kila mtu
aliyejiunga na mfuko huo anapo kuwa
inahitaji huduma ya dawa dawa hazikosekani zinakuwepo kwa pindi chote
Alisema indapo mtu atakuwa ameandikiwa dawa na
kukosekana kwenye zahanati na vituo vya afya mtu huyo atalazimika kwenda
kwenye hospitali teule ya Halmashauri ya
mji wa Mpanda na kupatiwa huduma hiyo ya dawa au kwenye maduka maalumu ambayo
yameteliwa kutowa huduma hiyo
0 comments:
Post a Comment