Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Mkuu wa Wilaya ya
Mpanda Paza Mwamlima amewaagiza viongozi wa Halmashauri ya Mji wa
Mpanda wahakikishe wanakwenda kwenye
mtaa kwa mtaa na nyumba kwa
nyumba kuwaelimisha watu wajiunge na mfuko wa bima ya Afya ya (NHIF)
Mwamlima
alitowa agizo hilo hapo juzi wakati wa uzinduzi wa huduma ya matibabu ya njia ya kadi (tika ) uzinduzi
uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Kakese
Alisema
kutokana na umuhimu wa huduma ya mfuko huo ni vema viongozi wakaacha
kukaa ofisi na waende kila mtaa kwa mtaa
na kuwaelimisha watu umuhimu wa kujiunga
na mfuko huo
Alifafanua kuwa hakuna nchi yoyote hapa duniani ambayo wananchi wake hawachangie hata
kidogo kwenye Serikali
yao
Alisema endapo
wananchi wataelimishwa
umuhimu wa kuchangia mfuko wa tiba kwa njia ya kadi(TIKA)
itawasaidia kwa ajiri ya maendeleo ya
afya zao
Awali kabla ya
uzinduzi wa huduma ya uzinduzi huo na
uzinduzi wa bodi ya mfuko wa bodi ya afya ya Halmashauri ya mji wa
Mpanda Meneja wa NHIF
wa Mikoa ya Rukwa na Katavi
Abdiel Mkayo alieleza kuwa hari ya uchangiaji kwa wananchi katika
mfuko wa afya wa afya kwa jamii tiba kwa kadi
sio ya kulidhisha na Mkoa wa katavi uko nyuma
Alisema kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya ya
Mpanda ni watu 1147 tuu wanachangia mfuko huo ambao ni sawa
na asilimia tatu na Halmashauri ya Wilaya ya Mlele inao wachangiaji 1,184 ambao ni sawa na asilimia tano
Mkayo
alieleza kuwa kwa upande wa Halmashauri ya Nsimbo ina jumla ya kaya elfu kumi na moja ambazo zinachangia mfuko
huo sawa na asilimia orobaini na saba
Alifafanua kuwa hadi kufikia Desemba mwaka huu
Serikali imepanga wananchi asilimia 30
wawe wamejuunga na mfuko huu na wawe
wanapatiwa matibabu kwa njia ya matibabu kwa njia ya kadi
Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Mji wa Mpanda Selemani Lukanga alieleza kuwa
wananchi waachane na mawazo ya kudhani kwamba mfuko wa bima ya afya upo
kwa ajiri ya watumishi tuu
Hivyo katika swala la afya watumishi hawaguswi
peke yao kwa hari hiyo wananchi wanao
wajibu wa kujiunga na mfuko wa bima ya
afya kwakuwa hakuna wananchi ambae haitaji huduma ya afya
Nae mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mpanda
Enock Gwambasa alieleza kuwa mwitikio wa
wanachi kujiunga na mfuko
huu ni mdogo sana kutokana na watu kuwasikiliza watu ambao sio wataalamu
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa bodi ya mfuko wa afya wa
Halmashauri ya Mji wa Mpanda Fotunata
Issaya aliwataka wananchi wa Halmashauri hiyo kujiunga na mfuko wa bima ya Afya
Alisema watu ambao watajiunga na mfuko huo watapata
matibabu ni sawa na bure kwani kiwango wanacho changia cha shilingi elfu kumi
kwa mwaka ni sawa na kupatiwa matibabu bure
0 comments:
Post a Comment