Home » » POLISI NA TANAPA WAKAMATA SMG NA RISASI 110 NA MAGAZINE MBILI ZIKIWA ZIMEHIFADHIWA ARDHINI MTUHUMIWA ATOROKA‏

POLISI NA TANAPA WAKAMATA SMG NA RISASI 110 NA MAGAZINE MBILI ZIKIWA ZIMEHIFADHIWA ARDHINI MTUHUMIWA ATOROKA‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
 Jeshi la Polisi  Mkoa wa Katavi kwa kushirikiana  na askari  wa Hifadhi  ya Taifa  ya wanyama poli  ya  Katavi(TANAPA)  wamefanikiwa kukamata  bunduki moja   aina ya SMG  ikiwa na magazine  mbili  na Risasi  110  za SMG  zikiwa  zimefishwa  katika Kijiji cha  Nzaga  kata ya Ulwira  Wilaya ya Mlele  Mkoa wa Katavi
Kamanda wa  Polisi wa Mkoa wa Katavi  Dhahiri Kidavashari aliwaambia jana  waandishi wa  Habari  kuwa  Askari hao walikamata silaha hiyo  hapo jana  majira ya saa  nane usiku kijijini  cha  Ulwira
 Alisema kabla ya tukio   Askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi na polisi  walipata  taarifa  kutoka kwa raia wema  kuwa kuna  mtuhumiwa   mmoja   jina limehifadhiwa mtuhumiwa  huyo  ambae ametoroka  kwa kuwa  bado anatafutwa  kuwa  anajishughulisha  na shughuli  za  ujangili  na anamiliki  silaha  moja  ambayo  inaitumia kwa shughuli hizo na ameifisha  shambani kwake
Hivyo  baada ya taarifa hizo kuwa zimepatikana  jeshi la  polisi kwa kushirikiana na TANAPA   walikwenda nyumbani kwa mtuhumiwa kwa lengo la kufuatilia tuhuma hizo
Kamanda  Kidavashari alisema  baada ya Askari hao kufika nyumbani kwa mtuhimwa  waliizingira  nyumba yake  na ndipo  walipoingia ndani  ya nyumba yake aliyokuwa akiishi na familia yake  walikuta ameisha toroka
 Alieleza  Askari hao walifanya upekuzi  na  walifanikiwa kukamata    bunduki moja  aina ya SMG  yenye  namba  C 2136 ikiwa na magazine mbili  pamoja na  risasi 110 za SMG  zikiwa  zimehifadhiwa ndani ya mfuko wa  salphet akiwa amezichimbia chini ya ardhi katika eneo la nyumba yake
Kamanda Kidavashari  alisema  pamoja na mtuhumiwa huyo kuwa ametoroka  juhudi  za kumtafuta  zinaendelea  pamoja  na kuwasaka  washirika  wanzake  ambao amekuwa akishilikiana nao kufanya  ujangili katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi na kwenye mapori ya akiba

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa