Home » » ZITO KABWE: HAKUNA KIONGOZI WA CHADEMA ALIWAHI KUTOA HOJA ILIYOWEZESHA KUMFUKUZA KAZI HATA MTENDAJI WA KATA

ZITO KABWE: HAKUNA KIONGOZI WA CHADEMA ALIWAHI KUTOA HOJA ILIYOWEZESHA KUMFUKUZA KAZI HATA MTENDAJI WA KATA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
Kiongozi  Mkuu wa  chama  cha  ACT   wazalendo    Zito  Kabwe amesema  kwamba viongozi wa  wanaongoza vyama vya siasa  hata  nchini  sio lazima watoke sehemu  moja  kama  ambavyo baadhi ya vyama vya siasa vinavyo fanya 
Kauli hiyo aliitowa hapo jana wakati alipokuwa akiwahutubia  wananchi wa Mji wa Mpanda  katika  mkutano wa hadhara uliofanyika  katika uwanja wa shule ya  Msingi  Kashaulili  mjini  hapa
 Zito   alisema  kumekuwa  na tabia ya vyama vya siasa  kutaka viongozi wa  ngazi za juu kutoka  katika Mkoa moja au  kanda moja na mapokeo yake anapo tokea mtu mwingine kutoka  mkoa mwingine  au kanda nyingine   hujengewa chuki na kuondolewa ndani ya chama
Alieleza ACT  wamuamua funya  ziara  katika  Mkoa wa Katavi kwa lengo la kukitambulisha rasmi  chama  hicho kwa  wananchi wa  Mkoa wa  Katavi
 Alifafanua wapo  baadhi ya viongozi wa vyama vya viasa kazi yao kubwa ni kupiga kele tuu  lakini hawana uwezo wa kujenga hoja za msingi  kwa wananchi  hivyo ni budi wananchi wakachambua pumba ni zipi na mchele ni upi
Naomba  kiongozi hata moja wa  CHADEMA  anieleze  ni hoja ipi ambayo aliwahi kutowa  na ikasabisha  hata  Mtendaji wa kata  akafukuzwa kazi  yeye  anaamini  hakuna  kiongozi hata moja wa  CHADEMA aliwahi  kujenga hoja hiyo alisema  zito  Kabwe na kushangiliwa na wananchi
pia  alizungumzia   sakata lake  na  sababu kubwa iliyomfanya afukuzwe kwa kuvuliwa nyadhifa zake na uanachama    kwenye  chama  cha  CHADEMA wakati  alipokuwa naibu  katibu  mkuu   Tanzania   Bara
 Alisema  sakata lake la lilianzia  toka  mwaka  2012 wakati  akiwa  ni mwenyekiti wa kamati ya  bunge ya ukaguzi wa fedha za Serikali
 Alifafanua  baada ya kuona  matumizi fedha  hayaendi vizuri kwenye  vyama  vya siasa  vilivyokuwa  vinapewa  ruzuku ya  fedha kutoka  serikali  alimwagiza mkaguzi mkuu wa   serikali avifanyie ukaguzi vyama vyote vinavyopokea ruzuku kutoka  Serikali  jinsi vinavyo tumia ruzuku hiyo
 Zito  alisema baada ya  kutowa maagizo hayo  aliitwa na  kamati kuu ya  CHADEMA  na   alihojiwa ni kwani  amaamua  kafanya  hivyo  kabla ya kukitonya  kwanza  chama chake
Alieleza kuwa  baada ya kuulizwa hivyo na wajumbe wa kamati kuu  aliwajibu kuwa  yeye  anachoangalia  ni utaifa kwanza mambo mengine  kwake huya yanafuata  hivyo aliamua kutowa maagizo hayo kwa  manufaa ya Taifa  sio kwa manufaa ya vyama
 Alisema baada ya kuwa  wanajua hawamuwezi kwenye  maswala ya kujibu hoja ndipo  walipoamua  kumuondoa kwa njia nyingine waliokuwa wanaijua wapo
Kwaupanda wake msanii  marufu  hapa  nchini  Afende  Sele  aliwataka  wakazi wa  Mkoa wa Katavi  kutoshabikia mambo ya siasa  kama ambavyo wanavyoshabikia timu za mpira
Mkutano huo ambao ulikuwa na watu wengi ulikuwa na ulinzi  mkali wa askari polisi  ambao walikuwa na sare  za jeshi hilo na wasio kuwa  na sere kufuatia  taarifa  ambazo zilikuwa zimeenea kabla ya mkutano huo kuanza kuwa kuna kundi linalodaiwa kuwa ni la wafuasi wa  CHADEMA walikuwa wamepanga  kumzomea  Zito wakati akihutubia lakini hari hiyo haikutokea

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa