Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter
Mguluchuma
Katavi yetu blog
Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Vestina
Peter(27) Mkazi wa Kijiji cha Ilalangulu Tarafa ya Mpimbwe Wilaya ya
Mlele Mkoa wa Katavi amekutwa akiwa ameuwawa kikatili kwa kuchomwa na visu
tumboni hadi utumbo wake kutoka nje
na kwenye sehemu ya bega lake na
watu wasiofahamika
Kamanda wa Polisi
wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari
aliwaambia waandishi wa habari kuwa tukio hilo la mauwaji ya kikatili
lilitokea hapo juzi majira ya saa kumi na mbili jioni
Alisema kabla ya tukio hilo marehemu aliaga
nyumbani kwake alikokuwa akiishi na mumewe
kuwa anakwenda shambani kwake kuimbua mahindi katika eneo la Kazaroho
Kidavashari
alieleza baada ya marehemu kuelekea huko shambani hakuweza kurudi nyumbani kwake kwa muda wa siku
mbili hadi hapo juzi
mwili wake ulipo onekana ukiwa
shambani kwake huku ukiwa amechomwa vifu
tumboni hadi utumbo wake kutoka nje
na akiwa na majeraha ya kuchomwa
na vifu sehemu ya kulia ya bega lake
Alisema baada ya mwili wa marehemu huyo kupatikani
taarifa zilitolewa kwenye kituo cha Polisi cha kibaoni ambao walifika
kwenye eneo hilo baada ya muda mfupi na chanzo cha mauwaji ya kikatili ya mwanamke
huyo bado hakifahamika.
Kamanda wa Polisi
Kidavashari alieleza mpaka sasa
jeshi la linawashikilia watu watu wawili
kwa mahojiano zaidi ambao ni Charles
Julio(42) Mkazi wa Ilembo na Fred
Ndaina (42) Mkazi wa Kijiji cha Ilalangulu Kata ya Kibaoni.
Alisema watuhuwa hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani
mara baada ya uchunguzi utakapo
kuwa umekamilika ili wakajibu tuhuma zinazo wakabili
0 comments:
Post a Comment