Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Watu watatu
wameonyesha nia ya kugombea ubunge wa Jimbo la Mpanda Mjini Mkoa wa Katavi (CCM) jimbo ambalo
linaongozwa na Mbunge Said Arfi (CHADEMA) aliyeliongoza jimbo hilo kwa kipindi cha miaka kumi sasa
Wanachama hao
walioanza harakati za kugombea jimbo
hilo ni Gabriel Mnyele
ambae ni mwanasheria maarufu
wa jijini Dares salaam
anaejishughulisha na kazi ya uwakili wa kuwashauri watu binafsi na makampuni
mambo ya kisheria
Mwingine ni
Sebastiani Kapufi ambae aliwahi
kuwa Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya
Mpanda kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia
mwaka 2007 hadi mwaka 2012 na pia aliwahi kuwa
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda kwa kipindi cha miaka mitano
Na
Galus Mgawe ambae kwa sasa ni meneja wa kampuni ya Aitel
wa Mikoa ya Mtwara , Songea na Lindi
Wagombea
wawili Galus Mgawe na Sebastiani Kapufi hii itakuwa ni kipindi chao cha tatu
kushiliki kwenye kinyang’ilo cha kugombea
ubunge kwenye kura za maoni za CCM
Uchaguzi Mkuu uliopita
wa mwaka 2010 CCM walimsimisha
kugombea ubunge wa jimbo hilo
Sebastiani Kapufi ambae alishindwa
na mbunge wa sasa Said Arfi (CHADEMA)
Jimbo la
Mpanda mjini lilikuwa halijawahi kuongozwa na mbunge
aliyeongoza jimbo hilo kwa vipindi viwili isipo kuwa Mbunge alipo sasa
ndiye aliyeweza kuongoza jimbo hilo ambalo lipo hati hati kurudi CCM kutokana na
mgawanyiko ulipo sasa ndani ya CHADEMA
katika jimbo la Mpanda Mjini
0 comments:
Post a Comment