Home » » HATARI SANA: MWALIMU WA SHULE YA MSINGI AUAWA KWA KUCHOMWA VISU

HATARI SANA: MWALIMU WA SHULE YA MSINGI AUAWA KWA KUCHOMWA VISU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter Mguluchuma
Katavi
Mtu  mmoja  aliyefahamika  kwa jina la  Mwita  Paulo (Ryoba) 25  mwalimu wa Shule ya Msingi Lukama Makazi ya Wakimbizi ya Katumba  Mkoa wa Katavi  ameuwawa  kikatili  kwa kuchomwa na  vifu  kifuani na watu wasio julikana
  Tukio la mauwaji hayo ya  kikatili ya mwalimu huyo  lilitokea hapo  juzi  majira ya    ya saa mbili na nusu  usiku  katika  eneo la  shule ya msingi  Mpanda  katika mtaa wa Mpanda Hotel  mjini hapa
Kamanda wa  Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi  Dhahiri Kidavashari  aliwaambia waandishi wa habari  kuwa   marehemu  kabla ya kifo chake hicho  aliaga kwenye  kituo chake cha kazi  katika shule ya Msingi Lukama  kuwa anakwenda mjini Mpanda  katika shule ya Sekondari ya Mwangaza kufanya mtihani wa  kidato cha sita
 Alisema  marehemu  alikuwa amefuatana na waalimu  wenzake ambao wanafundisha shule  za msingi mbalimbali zilizoko kwenye makazi hayo ya Wakimbizi ya Katumba ambao nao walikuwa wanakwenda kufanya mtihani wa kidato cha sita kwenye kituo cha kufanyia mtihani   katika shule ya Sekondari ya Mwangaza
 Kidavashari   alieleza  marehemu akiwa na waalimu  hao  aliweza kufika katika shule ya mwangaza   na  kufanya mitihani yake  ambapo alikuwa akirudia kufanya mtihani ya  baadhi ya masomo  ambayo hakuwa amefanya  vizuri  katika masomo yake ya kumaliza kidato cha sita
 Baada ya kumaliza mitihani waalimu wenzake  walianza safari la kurejea kwenye vituo vyao vya kazi  katika makazi ya wakimbizi ya Katumba  lakini yeye aliamua kubaki mjini Mpanda
 Alisema  baada ya hapo marehemu  Mwita  Paulo  hakuonekana  tena  mpaka mwili wake  ulupoonekana  katika  eneo la shule ya Msinngi Mpanda    mtaa wa Mpanda Hotel  huku ukiwa  amechomwa vifu  katika sehemu zake za kifuani
 Kamanda  Kidavashari  alisema  chanzo cha tukio hilo bado hakija fahamika na  hakuna mtu wala watu waliokamatwa kuhusiana na tukio  hilo na polisi wanaendelea na  uchunguzi  wa kifo cha mwalimu huyo
    

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa