Home » » WAANDISHI WA HABARI WAPEWA SOMO KUHUSU MAPAMBANO YA RUSHWA

WAANDISHI WA HABARI WAPEWA SOMO KUHUSU MAPAMBANO YA RUSHWA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter   Mguluchuma
Katavi
 Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Katavi  wameelezwa   kuwa  majukumu makubwa  ya TAKUKURU  ni  kuzuia rushwa  na  kutowa elimu  kwa wananchi  juu ya rushwa  na kupambana na rushwa  
Hayo yalisemwa hivi karibuni  hivi na Mratibu  wa dawati la  elimu  kwa umma  wa TAKUKURU wa Mkoa wa Katavi  Everist Ndongolo     kwenye semina ya waandishi wa Habari wa Mkoa wa Katavi  iliyoandaliwa na TAKUKURU Mkoa wa Katavi iliofanyika  katika ukumbi wa  jengo la Ofisi ta Takukuru Mjini hapa
 Ndogolo  alieleza  kuwa  TAKUKURU imeandaa semina hiyo ya siku  moja   kwa lengo  kueleza  jitihada zinazofanywa  na     Serikali  kuhusu mapambano dhidi ya Rushwa
Alisema  majukumu  makubwa ya TAKUKURU   ni kufanya kazi ya kuzuia rushwa , kutoa elimu  juu ya rushwa  na kupambana na Rushwa
 Alifafanua kuwa  katika kuzuia rushwa kunahusisha  utafiti na   katika kutoa elimu   kunahusisha  mikutano ya hadhara  na kupitia  club  za  shule  na vyuo
Ndogolo  alieleza kuwa zipo aina kuu mbili za rushwa ambazo alizitaja kuwa   kuna rushwa kubwa  na rushwa ndogo
 Alisema rushwa ndogo huwa zinawagusa  watu au mtu mmoja mmoja  pamoja na viongozi wa ngazi ya chini  na Rushwa kubwa inawgusa viongozi wa  wakubwa
 Alitaja baadhi ya sababu  zinazopelekea  kuwepo kwa rushwa  katika jamii  kuwa ni kupanda kwa gharama  za maisha ,sheria zilizopitwa na wakati  pamoja na mazoea waliyojizoweshea wananchi kwa watumishi  kwamba  bila kutoa chochote  hawezi kutimiziwa kile  ambacho  anakihitaji
Nae Mkuu wa TAKUKURU  wa Mkoa wa Katavi  Cristopher Nakua alisema kuwa taasisi  hiyo ya kuzuia na kumbambana na rushwa imekuwa ikikutana   na changamoto mbalimbali
 Nakua alitaja baadhi ya   changamoto  kuwa ni  wananchi  kutotowa   na ushilikiano  wa kutosha kwa TAKUKURU  hali  ambayo imekuwa  ikirudisha nyuma  ufanisi  wa utatuzi  wa  masuala  ya Rushwa
Mkuu huyo wa TAKUKURU wa Mkoa wa Katavi alitowa  wito  kwa wananchi wa Mkoa wa Katavi  viashiria vya   kuwafichua  au kutoa taarifa  zinazoleta  viashiria vya Rushwa katika  sehemu mbalimbali na katika sehemu zao za kazi

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa