Home » » AKAMATWA NA SILAHA BUNDUKI YA KIVITA AINA YA AK 47 NA GOBORE

AKAMATWA NA SILAHA BUNDUKI YA KIVITA AINA YA AK 47 NA GOBORE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi linamshikilia mtu mmoja mkazi wa kijiji cha  Mazigo Tarafa ya Inyonga  Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi kwa tuhuma za kumkamata na  silaha bunduki ya kivita aina ya AK 47  na Gobore moja
Mtuhumiwa huyo aliyekamatwa ametajwa kuwa ni  Emanuel  Herman (KAMTUPE) 36 ambae ni mkazi wa Kijiji cha Masigo Tarafa ya Inyonga Wilaya ya Mlele Mkoani  hapa
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari alisema kuwa  tukio la kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo na silaha hizo mbili lilitokea hapo juzi majira ya  saa nane usiku  katika  Kijiji hicho cha Masigo
Kidavashari alisema  mtuhumiwa huyo alikamatwa kufuatia taarifa za kutoka kwa raia wema walilizozitowa kwa askari wa wanyama poli kuwa mtuhumiwahuyo amekuwa akimiliki  silaha kinyume cha sheria na amekuwa akizitumia kwa uwindaji haramu
Baada ya taarifa hizo  kuwafikia askari wa wanyama poli  walianza msako wa kumsaka mtuhumiwa huku wakiwa wanaongozwa na Afisa wa wanyama pori  Cedrick  Mashauri
 Kidavashari alieleza  katika  msako wa askari  wa wanyama poli  hao walifanikiwa hapo juzi kumkamata mtuhumiwa  Emanuel  Herman(KAMTUPE) akiwa   silaha  bunduki mbili  moja aina ya   AK 47   na  nyingine  aina ya Gobore
 Alisema mtuhumiwa alikuwa akimiliki  bunduki hizo  kinyume cha sheria na  alikuwa akizitumia kwa   ajiri ya uwindaji haramu katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi na kwenye mapori ya akiba
Mtuhumiwa bado anaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi na anatarajiwa kufikiwa mahakamani mara baada ya uchunguzi utakapo kuwa umekamilika  aliwaambia waandishi wa habari Kamanda Kidavashari
 Hivi karibuni Askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi  waliweza kufanya doria na kufanikiwa kuwakamata watu watatu wakiwa na vipande vitatu vya meno ya Tembo  yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 11 ambayo walikuwa wakitaka kuyasafirisha kutoka kwenye Makazi ya  Katumba Wilaya ya Mlele  kuyapeleka  Mkoa wa Tabora

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa