Home » » WASHIKILIWA NA POLISI KWA KUKAMATWA NA NYAMA YA KIBOKO

WASHIKILIWA NA POLISI KWA KUKAMATWA NA NYAMA YA KIBOKO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter Mguluchuma
Katavi
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi   linawashikilia watu  watu wawili wakazi  wa Kijiji cha  Masigo Tarafa ya Inyonga Wilaya ya  Mlele  kwa tuhuma ya kuwakamata na nyama ya kiboko  zaidi  ya kilogramu 50 katika  matukio mawili tofauti
Watuhumiwa hao waliokamatwa wametajwa kuwa ni  Ramadhan Majengo(66)   Emanuel  Herman(36)wote wakazi wa Kijiji cha Mazigo Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi 
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari aliwaambia waandishi wa Habari jana  kuwa  tukio  la kwanza la kukamatwa kwa watuhumiwa hao wawili  wakiwa na nyama   ya kiboko lilitokea hapo juzi
Katika tukio hilo ambalo lilitokea  majira ya saa sita na nusu   askari  wa Wanyama pori  ambao waliokuwa doria  wakiongozwa  na  Askari mwenzao  Cedrick  Mashauri  walimkamata mtuhimwa  Ramadhani  Majengo akiwa na nyama ya Kiboko  kilo 40  akiwa  nyumbani kwenye Kijiji cha Mazigo
Kamanda Kidavashari aliwaambia waandishi wa Habari kuwa  mtuhumiwa huyo alikamatwa kufuatia taarifa za kutoka kwa raia wema ambao walitowa taarifa kwa askari wa wanyama poli kuwa  mtuhumiwa huyo alikuwa akijihusisha na uwindaji haramu wa wanyama kwenye Hifadhi ya Taifa ya Katavi na kwenye mapori ya akiba
Alisema tukio la pili la kukamatwa kwa watuhumiwa hao lilitokea hapo jana majira ya  saa saba usiku huko katika eneo la Kijiji cha  Mazigo Tarafa ya Inyonga Wilaya ya Mlele
 Katika tukio hilo A skari wa Wanyama poli ambao walikuwa wakifanya dolia walimkamata mtuhumiwa  Emanuel  Herman akiwa na nyama ya  Kiboko  kilogramu 15 ambazo zilikuwa zimebanikwa
Kidavashari alisema watuhumiwa hao wote wawili wanaendelea  kushikiliwa na jeshi la Polisi na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani  mara baada ya uchunguzi utakapo kuwa umekamilika
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi  ametowa wito  kwa Wananchi  wale ambao wanajihusisha  na biashara  haramu  ya nyara za Serikali  waache  mara moja  kwani kufanya hivyo ni kinyume   cha sheria  na  zinasababisha  hasara  na uharibifu mkubwa wa  rasilimali  za Taifa

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa