Home » » KATAVI KUZINDUA HUDUMA YA UZAZI WA MPANGO‏

KATAVI KUZINDUA HUDUMA YA UZAZI WA MPANGO‏


Walter  Mguluchuma
Katavi
Maelfu  ya Wakazi wa  Mkoa wa Katavi  leo  watajumuika  na Marie  Stopes   Tanzania (MST) katika viwanja vya shule ya Msingi Kashaulili mjini  Mpanda  kusherekea  uzinduzi  wa huduma  ya uzazi  wa  mpango  na pia  watapatiwa huduma  hiyo bure
 Sherehe hizo za uzinduzi wa  wa uzazi wa Mpango  ambazozimevutia hisia za watu wengi wa Mkoa  wa  Katavi na Wilaya zote za Mkoa huu zinatarajiwa  kuzinduliwa na  Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dr Ibrahimu Msengi ambae atawakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima ambae atamwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Katavi
Kwa mujibu  wa taarifa ya  mkuu wa  kitengo  cha  mahusiano  na mawasiliano  wa MST  leo  Brant  aliyoitowa kwa waandishi wa habari sherehe hizo zinatatajiwa  kuzindiliwa  leo majira ya saa nne asubuhi  katika uwanja huo
  Tukio  hili la uzinduzi wa mradi  mkubwa wa  kutoa huduma  bure  za  uzazi wa  mpango  umuisha fanyika katika Mikoa mbalimbali hapa  nchini 
Lengo  la uzinduzi huo ni  kuhamasisha  kampeni  mahususi  ya Marie  Stopes  ijilikanayo  kama  changua  maisha
Huduma  zinazotolewa  kupitia  shirika  la Marie  Stopes  zinachangia  asilimia  ishirini na tano  ya huduma zote  za  uzazi wa  mpango  ukiondoa kondomu
Kwa upande wake mkazi wa Mtaa wa Kawajense Said Juma ameeleza kufurahishwa na  uzinduzi huo wa mpango wa uzazi katika Mkoa wa Katavi
Alisema mpango huo utawasaidia  kuweza kuwa na mpango mzuri wa uzazi kuliko ilivyo sasa kwani familia nyingi katika Mkoa wa Katavi zimekuwa azifuati mpango wa uzazi na matokeo yake wamekuwa wakishindwa kuwapatia huduma za msingi watoto wao kama vile kuwapeleka shule

       
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa