Home » » WANAWAKE 255 WAFA KUTOKANA NA MATATIZO YA UZAZI

WANAWAKE 255 WAFA KUTOKANA NA MATATIZO YA UZAZI


N a  Walter  Mguluchuma
Katavi
Jumla ya Wanawake  255  wamefariki Dunia  Mkoani Katavi katika kipindi cha mwaka 2014  kutokana na  matatizo ya uzazi  kwa kila  vizazi hai  laki moja
 Hayo yalielezwa hapo jana na Mkuu wa Mkoa wa  Katavi Dr  Ibrahimu  Msengi  kwenye hotuba yake ya uzinduzi  wa  huduma za  uzazi  wa mpango  iliyosomwa kwaniaba yake na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi Paza Mwamlima ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda  kwenye sherehe ya uzinduzi huo iliofanyika katika uwanja wa shule ya Msingi Kashaulili mjini Mpanda na huhudhuriwa na maefu ya wakazi wa Mkoa wa Katavi
 Alisema Katika Mkoa wa Katavi  kiwango  cha  vifo  vya wanawake  vinavyotokana  na matatizo  ya uzazi kwa kipindi cha mwaka jana wa 2014  ilikuwa   ni 255 kwa kila  vizazi hai  laki moja  
 Idadi  hii ni kwa wale  wanawake  waliotolewa  taarifa  katika vituo  vya kutolea  huduma  na kutoka  katika  ngazi ya  jamii hivyo idadi hiyo inaweza ikawa ni kubwa zaidi kwani  ziko taarifa nyingine za vifo vya wanawake taarifa zake hazitolewi   kwenye ngazi husika hasa kwenye maeneo ya vijijini ambako  kunafikika kwa shida
Dr  Msengi alieleza  kiwango  cha Kitaifa  cha  vifo  vya wanawake  vinavyotokana  na matatizo  ya uzazi  ni  454 kwa  kila vizazi hai  laki moja
 Utafiti kuhusu  afya ya uzazi wa mwaka 2010 (Tanzania  Demographic Survery) inakadiliwa  kuwa  asilimia  23 ya wanawake  wenye umri  wa miaka 15 mpaka  19 na asilimia  54 ya  wenye umri   wa miaka 19 mpaka  24  tayari wana watoto  na mimba  katika umri  mdogo huchangia  vifo  mara  mbili  hadi tano  ya vifo vitokanavyo  na uzazi
 Alisema  kiwango cha  utumiaji  wa njia  za uzazi  wa mpango  katika  Mkoa wa   Katavi  kwa mwaka 2014 ilikuwa ni asilimia 38.4 tu  kiwango   hicho  kiko chini  sana  ukilinnganisha na kiwango cha  Kitaifa  kwani kiwango cha  Taifa ni asilimia sitini
Dr Msengi alieleza  wapo watu wanaamini kuwa  kuzaa watoto wengi  ni utajiri  na wengine wanaamini  mwanamke  ni chombo  cha kuzaa watoto tuu  hivyo ni vizuri watu wakaepukana na mila hizo potofu
Kwa upande wake  Mkurugenzi Mkuu wa  Rasilamali watu  wa Marie  Stopes  Tanzania (MST) Eliy Reweta ambae alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu alieleza kuwa  Marie Stopes  inatowa huduma hiyo ya uzazi  wa mpango wa  bure  lengo   ni  kumwezesha kila   mmoja  kuchagua  njia  ya uzazi  ya mpango  anayohitaji  hasa miongoni  mwa vijana
Alifafanua kuwa vijana  wanaweza  kudhani  kuwa huduma  za uzazi  wa mpango  ni kwa ajiri ya  watu wanaoishi katika ndoa  wakati ni muhimu wao  kuepuka  mimba  zisizotakiwa  hata kabla ya ndoa
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mpanda Enock  alisema kuwa  uzazi wa mpango  ni jambo la muhimu sana kwenye maisha ya Binadamu kwani husaidia  kupunguza vifo vya watoto  wachanga ambao mama zao hupata ujauzito wakati wakiwa bado wadogo
 Alisema pia uzazi wa mpango husaidia  watoto  kuzaliwa kwa  kuachiana nafasi na kunyonyeshwa kwa muda  wa miezi inayotakiwa na mama zao   
Nae  mshindi wa  taji la  Miss Marie Stopes katika mashindano  ya Miss  Tanzania  yaliofanyika mwezi Septemba mwaka jana   Doreen  Benne  alieleza kuwa  uzazi wa mpango  unamkinga mwanamke  asipate mimba  zisizotarajiwa  na  kumwepusha  na kuingia kwenye mtego wa kutowa mimba  kusiko salama
Napia  uzazi wa mpango  unamsaidia mwanamke  kuishi maisha  mazuri  yale ambayo  anayoyataka mwenyewe  kadri atakavyo kuwa amejipangia mwenyewe  alisema Doreen
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa