Home » » MPANDA WAZINDUA BARAZA LA BIASHARA LA WILAYA‏

MPANDA WAZINDUA BARAZA LA BIASHARA LA WILAYA‏

 Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
 Mkuu wa Wilaya ya Mpanda  Paza   Mwamlima  amezindua  rasmi    Baraza la  Biashara  la Wilaya ya Mpanda   lenye lengo la kuwaunganisha wafanyabiashara na Serikali
Mwamlima  alizindua baraza hilo la  biashara hapo jana  katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mpanda ulioko  katika  enep la Ilembo   mjini  hapa
Katika hutuba yake ya uzinduzi huo    Mwamlima aliwaeleza wajumbe wa baraza hilo kuwa  baraza hilo limeundwa   na wajumbe ishirini kutoka Serikalini  na  ishirini kutoka Sekta  binafsi  ambapo mwenyekiti wa baraza hilo ni yeye Mkuu wa Wilaya
 Alisema miongoni  mwa malengo ya  baraza hilo ni kuunganisha Serikali na  taasisi  binafsi  ili kuwaelimisha wananchi wafanyabiashara watambue umuhimu wa kulipa kodi  kwani wafanyabiashara wasipo  lipa kodi nchi haiwezi kuendelea
 Alifafanua kuwa  kwa nchi changa mfanyabiashara  ambae anakwepa kulipa kodi anajiona ni  mjanja wakati kwa nchi zilizoendelea swala la kulipa kodi ni lalazima na sio hiyari
Mwamlima  alisema chombo hicho kinaowajibu  wa kumuinua  mwananchi  kwa  kumsaidia  kwa kumuelimisha  kibiashara  na kumfanya aongeze kipato chake
Dc huyo aliwataka wajumbe wa Baraza hilo  kuhakikisha wanaondoa  migogoro yote ya wafanyabiashara  na kuwatafutia  masako ya mazao  yao ndani ya nchi na nje ya nchi yetu ya Tanzania
 Alisema  viongozi wa Wilaya ya Mpanda   wamekuwa wakitumia  muda mwingi  na gharama kubwa kushughulikia  migogoro  hivyo  baraza hilo litawapunguzia mzigo huo  viongozi wa Serikali  na kuwafanya washughulikie  zaidi shughuli za maendeleo  badala ya migogoro
Kwa upande wake afisa mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Phosphor  Nsuri  alieleza kuwa  Wilaya ya Mpanda imekuwa ikipokea  wageni wengi wanaohamia kwenye Wilaya hiyo kwa kasi kubwa kutokana na furusa  mbalimbali zilizopo katika wilaya hiyo
Alizitaja baadhi ya furusa hizo kuwa ni  madini  utalii  kilimo  ufugaji   uvuvi  katika mwambao mwa ziwa Tanganyika
Nae katibu wa  Baraza hilo Askofu Labani Ndimubenya alisema  kuwa   Baraza hilo  litahakikisha  linaimarisha mawasiliano  ya ngazi ya Wilaya na ngazi ya Mkoa 

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa