Home » » HOT NUUUUZ: AKATWA NA PANGA BAADA YA KUFUMANIWA AKIFANYA MAPENZI NA MKE WA MTU JIKONI , SOMA HAPA

HOT NUUUUZ: AKATWA NA PANGA BAADA YA KUFUMANIWA AKIFANYA MAPENZI NA MKE WA MTU JIKONI , SOMA HAPA

Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi  linamshikilia  Deocratias   Pastory (30) Mkazi wa Kijiji  cha   Ntumba Wilaya ya Mpanda  kwa tuhuma za kumjeruhi vibaya tumboni kwa kumkata na panga  hadi utumbo kutoka nje   Masanga  Elias(28) Mkazi wa Kijiji cha Stalike  Tarafa ya Nsimbo baada ya kumfumania akifanya mapenzi (tendo la ndoa)   jikoni  na mke wake  
Kwa   mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Kamishina msaidizi mwandamizi  Dhahiri Kidavashari  aliwaeleza waandishi wa habari ofisini kwake kuwa tukio hilo  lilitokea  hapo  Machi  29   majira ya saa tano usiku katika Kijiji  cha  Kapanga Wilaya ya Mpanda  nyumbani kwa mtuhumiwa  Deocratias
Kamanda Kidavashari  alisema siku hiyo ya tukio  majira ya mchana  mtuhumiwa  aliaga  nyumbani kwake  kuwa  anaelekea  katika Kijiji  cha  Kapanga kwa ajiri ya  shughuli  za  shambakwa kutumia usafiri wake  wa  baiskeli
 Alieleza wakati akiwa njiaani akiendelea  na safari yake baiskeli yake aliyokuwa anaitumia iliharibika  na  hakuwa na namna yoyote ile ya kuitengeneza
Ndipo mtuhumiwa alipoamua  kuanza safari ya kurudi nyumbani  ambapo aliweza kufika nyumbani kwake walikokuwa wakiishi na mkewe muda wa saa tano usiku
Kidavashari alisema  baada ya kufika nyumbani  alimkuta mke wake  aitwaye  Tabu   Nestory(20) akiwa  anafanya mapenzi  (tendo la ndoa)  jikoni na mtuhumiwa  huku  akimtamkia kuwa anampenda  sana
 Alisema kitendo hicho cha kumfumania mke wake akifanya tendo la ndoa na mtuhumiwa  huku  mkewe akimwambia mtuhumiwa  kuwa anampenda sana kilimkasilisha  sana mtuhumiwa  Deocratius   Pastory
Ambapo kitendo hicho kilisababisha  mtuhumiwa  kuanza  kumshambulia  Masaga  Elias kwa kumkata na panga tumboni   hadi utumbo kutoka nje  ambae  muda huo alikuwa bado akiendeku kufanya tendo la ndoa  na huku  mtuhumiwa  akiwa na shuhudia 
Alisema  kisha mtuhumiwa baada ya kuwa amemjuruhi vibaya mgoni wake   alimkata mkewe kwa panga    kwenye mkono wake wa kushoto   hari  ambayo  ilimfanya mkewe apige kelele ya kuomba msaada kwa majirani  na majirani walifika kwenye eneo hilo baada ya muda mfupi
Kamanda Kidavashari   alisema  mpaka sasa  majeruhi   Deoctatius  Elias bado   amelazwa  katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda akiwa anaendelea kupatiwa matibabu haku hari yake ikiwa mbaya
Amewaasa  wanandoa  wawe na tabia ya kuheshimiana  na kufuata  maadili  yanayokubalika na Dini  na jamii  ili kuepusha  migogoro ya nanma hii  na  pindi  inapojitokeza  wahusika  wajitahidi  kutoa taarifa  kwenye vyombo vya sheria  ama  mamlaka  zilizokasimishwa  kusuruhisha migogoro  ya wanandoa  badala ya kujichukulia sheria  mikonon


    


Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa