N a Walter Mguluchuma
Katavi
Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu ya Tanzania
Kanda ya Sumbawanga Jaji Kakusulo Sambo amewataka Mahakimu
watambue kwamba kazi ya msingi ya Mahakama ni kutoa
haki
Kauli hiyo aliitowa hapo jana wakati alipokuwa
akifungua kikao cha Baraza la wafanyakazi la kanda ya
Sumbawanga lililofanyika katika ukumbi wa idara ya maji Mjini Mpanda Mkoa
wa Katavi
Alisema katiba ya nchi yetu ipo
wazi na inaeleza kwamba chombo chenye mamlaka ya
kutoa haki ni wajibu wa Mahakama ya Tanzania
Jaji Sambo alieleza kila
Hakimuanaowajibu wa atekeleze malengo na
maagizo yaliopo kuhusu utoaji haki yaani
usikilizaji wa mashauri
Alisema kwa hiyo jambo
lolote linalipelekea kukwamisha utoaji wa
haki liogopwe kama ukoma na viongozi wa maeneo husika
walishughulikie haraka
Alieleza Mahakama za mwanzo na vikao
vya mahakama kuu kwa kesi za mauwaji huendeshwa kwa
kushilikiana na wazee washauri(wazee wa baraza)
Alisema hawa waheshimiwe sana
tuwajali vinginevyo mahakama itashindwa kuteleza
jukumu lake la msingi endapo wataamua kutoshirikiana
vyema na mahakama au wakigoma
Alisisitiza kuwa walipwe posho
zao haraka na kwa umaakini mkubwa ili kuondoa
malalamiko yasiyo na msingi au ulazima wa kutokea
Alifafanua kwasasa Mahakama haina
tatizo la ukosefu wa fedha za kuwalipa washauri hao
hivyo watumisha ambao wanawaandalia malipo wafanye kazi hiyo bila
kusukumwa
Ni marufuku na mwiko kwa pesa
zinazoletwa kwa ajiri ya kuwalipa washauri kuzitumia
kwa shughuli nyingine yoyote ile hata ikiwa nzito kiasi gani
aliagiza jaji huyo
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment