Home » » RAIA WAPYA 56,554 KATI YA 62,544 WANAISHI KWENYE MAKAZI YA WAKIMBIZI YA KATUMBA WAMEPTEWA VYETI VYA URAIA

RAIA WAPYA 56,554 KATI YA 62,544 WANAISHI KWENYE MAKAZI YA WAKIMBIZI YA KATUMBA WAMEPTEWA VYETI VYA URAIA


Na  Walter Mguluchuma
Katavi
 Jumla ya  Raia wapya  56,554 waliokuwa Raia wa Burundi  kati  ya  62,544 wanaoishi  katika makazi ya Wakimbizi ya Katumba  Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi   wamepatiwa vyeti vya  urai wa Tanzania
Hayo yalielezwa  hapo jana na  Afisa  Maendeleo ya Jamii    toka Ofisi ya Katibu  Tawala wa  Mkoa wa Katavi  Ignas Kikwala katika taarifa aliyoisoma  kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi  kwa  wakati wa  kikao cha  sita cha  kamati ya ushauri  ya Mkoa wa  Katavi(RCC)kilichofanyika katika ukumbi wa idara ya maji mjini  hapa
Alisema  Mkoa wa Katavi una kambi mbili za Wakimbizi ambazo ni Katumba  na Mishamo  hadi kufikia  Novemba 30  mwaka  jana  Makazi ya Katumba yalikuwa  na wakimbizi 76,769 kati hati ya hao  62,544 walikubaliwa  kupewa uraia wa Tanzania
 Waliokataliwa kupewa uraia ni  2150 wanaopaswa  kurejea  Burundi  kwa hiari yao  toka mwaka jana lakini wamekuwa wakikwepa  kurejea kwao  kwa sababu mbalimbali
 Alifafanua  wakimbizi ambao hawakusajiriwa 647wakimbizi ambao  hawakunyimwa Uraia  wala kukataliwa ni  218 na Wakimbizi  ambao fomu zao zilikuwa na matatizo ni ishirini
 Kikwala  alisema  kwa upande wa Makazi ya Mishamo  Watanzania wapya  waliopewa uraia  ni  52,594 waliokataliwa  ni 1155 wanaopaswa kurejea kwao Burundi  kwa hiari ni  2500 na wamekuwa wakikwepa kurudu kwa kudhania kuwa na wao watapewa Urai wa Tanzania
  Hivyo  kufanya  jumla ya   Raia  wapya wa Tanzania  katika Mkoa wa Katavi  watakaopewa  vyeti  vya uraia  kuwa ni  115,138
 Kwa upande wa wake mkuu wa Makazi ya Wakimbizi ya Katumba  Athumani  Igwe alieleza kuwa  hadi kufikia Februari  20 mwaka huu  jumla ya  Raia  wapya  waliokuwa wamepewa  vyeti  vyao vya uraia  ni 56,554 kati ya  62,544 katika Makazi ya Wakimbizi ya Katumba  sehemu  ambayo  zoezi la  ugawaji wa vyeti limekamilika  kwa sasa
 Alisema    raia wapya  3692 hawakupewa vyeti vyao vya uraia   kwa sababu mbalimbali  ambapo wengine walikuwa ni wagonjwa na wengine walikuwa masomoni hivyo utaratibu wa kuwapatia vyeti vya uraia unaandaliwa  kabla ya zoezi hilo kukamiika  katika  Makazi ya Mishamo
 Kwa sasa  zoezi hilo  la ugawaji wa vyeti unaendelea katika   ya Ulyankulu  Mkoa wa Tabora  baada ya  kukamilika  katika makazi hayo  zoezi  litahamia  katika Makazi  ya Mishamo Mkoa wa Katavi  na  linategemea  kukamilika Apri 30 nwaka huu
 Aidha katika kikao hicho Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini alishauri kuwa  maeneo hayo yaliokuwa ya Makazi ya wakimbizi  yanapaswa kuwa ni maeneo ya  makazi ya watu kutokana na mahitaji ya ardhi kwa watu kwa sasa
Alisema kwani kabla ya maeneo hayo ya kuwa makazi 1972  yalikuwa ni maeneo ya hifadhi ya mistu   hivyo Serikali ione  nanma ya kubadili matumizi ya eneo hilo


Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa