Na Walter Mguluchuma
Mkuu wa Mkoa
wa Katavi Dkt Ibrahim Msengi ameagiza wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Katavi
kuakikisha wanawaondoa watu wote ambao wanaoishi kwenye vyanzo
vya maji na maeneo amabayo hayakurusiwa kuishi na wakuu wa Wilaya wawasimamie wakurugunzi
wao kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa.
Dk Msengi
ametoa agizo hilo wakati wa kikao cha ushauri wa Mkoa wa Katavi kilichofanyika jana kwenye ukumbi wa idara ya maji mjini hapa
Amewataka
wananchi wote kuzingatia sheria,kila Mtendaji
lazima asimamie sheria na wawajibike kwa kusimamia sheria zilizopo,wasiwe na
woga wa kuwaonea aibu wananchi katika usimamiaji wa sheria.
Kutokana na
hilo amewaagiza Wakuu wote wa Wilaya kuwasimamia wakurugenzi kuhakikisha
wanasimamia sheria kuwa kuwaondoa wale wote wanaoishi maeneo ambayo ni kinyume
cha sheria kwa kuwa wameenda kukaa huko kinyume na sheria kila mmoja lazima
afuate sheria, na kila mtendaji awajibike kwa nafasi aliyonayo
Wajumbe wa
Kikao hicho wameshauri kuwa shughuli za
kisiasa na za kiutendaji ni vyema
zikatenganishwa ili kufuata sheria katika kutekeleza shughuli za serikali na
wananchi wafuate sheria.
Akichangia
katika kikao hicho Padri wa Kanisa Katoliki ambaye ni Msaidizi wa Askofu Jimbo
la Mpanda Kanisa Katoliki Padri Patrick
Kasomo ameeleza kuwa migogoro mingi ya ardhi na mipaka ya vijiji inasababishwa na kutanguliza siasa wakati wa
utekelezaji wa sheria.
Akashauri
kuwa wale waliopewa mamlaka ya kusimamia
sheria na mipaka wanafahamika ni watendaji na siyo wanasiasa,akataja baadhi ya
maeneo ambayo wananchi wana migogoro na wameanzisha vitongoji kiholela,akataja
kijiji cha Kapalamsenga kuwa kuna migogoro ya mipaka kwenye vitongoji.
Awali Mbunge
wa Jimbo la Mpanda Mjini Said Alf alishauri wataalam wasiadie kusimamia na kuainisha
maeneo ya vijiji nay ale yanayodaiwa kuwa na migogoro iainishwe.
Charles
Kanyanda Msaidizi wa Mbunge Jimbo la Katavi alishauri kuwa migogoro ya vijiji
serikali ianishe na kuweka mipaka ili
kuondoa migogoro hii, ili kuweza kuepuka.
Naye Mbunge
wa Jimbo la Mpanda Magharibi Moshi Selemani
Kakoso alieleza kuwa migogoro mingi iliyopo kwenye baadhi ya vijiji wilayani
mpanda kwa vijiji kumi vilivyopo kwenye Hifadhi ya wanyamapori ya vijiji inasababishwa na WMA.
Kakoso
alisema mbali ya migogoro hiyo ameeleza kuwa vyanzo vya maji vilivyoko kwenye
Kata ya Katuma kata ambayo ni ndiyo vilipo vyanzo vingi vya maji ambavyo ni
muhimu na tegemeo la wakazi wa mkoa wa Katavi na Hifadhi ya wanyamapori ya
Katavi imevamiwa na wafugaji na kuharibu vyanzo hivyo.
Kwa upande
wake Mkuu wa Makazi ya wakimbizi Katumba alieleza kuwa eneo la makazi ya
wakimbizi ya Katumba vijiji vimeanzishwa ndani ya makazi hayo kiholela hali
ambayo ni uvunjifu wa sheria.
Awali Katibu
Tawala wa Mkoa Mhandisi Emanuel Kalobelo aliwaagiza watendaji wote kuainisha makazi
yote holela, na mifugo iliyopo kwenye mkoa ili kufahamu idadi ya wakazi na
mifugo iliyokopo katika mkoa na kufahamu idadi ya makazi holela.
Akawata
Wakurugenzi kuhakikisha wanasimamia sheria kuwa kuwaondoa
wale wote wanaoishi maeneo ambayo ni kinyume cha sheria kwa kuwa wameenda kukaa
huko kinyume na sheria kila mmoja lazima afuate sheria, na kila mtendaji
awajibike kwa nafasi aliyonayo.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment