Na Walter Mguluchuma
Katavi
Wauguzi wa Halmashauri ya Mji wa Mpanda Mkoa wa Katavi wametakiwa kutimiza wajibu wa kazi yao na wawe wanawatolea lugha nzuri akina Mama wajawazito wanapokuwa wanawahudumia
Wito huo ulitolewa hapo juzi na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mpanda Yusuph Ngasa wakati alipokuwa akiwahutubia wauguzi wa kituo cha Afya cha Mpanda Mjini kwenye afla fupi ya kupokea msaada wa vitanda vitano vyenye vya kujifunglia akina Mama wajawazito vya thamani ya shilingi milioni tano vilivyotolewa na Benki ya NMB
Ngasa alisema wapo baadhi ya wauguzi wamekuwa wakiwatolea lugha za matusi akina Mama wajawazito wanao kwenda kujifungua hari ambayo inawafanya akina mama wajawazito waache kujifungulia kwenye vituo vinavyotowa huduma ya uzazi na kuamua kujifungulia majumbani
Alieleza kuwa endapo Wauguzi watatimiza wajibu wa kazi yao itawasaidia wao kupunguza lawama za akina mama wajawazito zisizo na lazima
Alifafanua ili wauguzi waweze kupunguza lawama zisizo na lazima za malalamiko ya akina Mama wajawazito njia pekee ni wauguzi kufanya kazi kwa kutimiza wajibu wa kazi zao
Alisema akina Mama wanapaswa kuonewa huruma kwani matatizo mengi yamekuwa yakiwakuta wanawake kuliko wanaume kwani wao ndio wanaolea watoto hadi kukua
Ngasa alieleza kuwa kumekuwa na tabia ya wanaume waliowengi kukataa kwenda huhudhuria kiliniki na wake zao na matokeo yake wamekuwa wakiwaacha wake zao kwenda peke yao
Umefika wakati sasa wanaume wabadilike na wawe na tabia ya kwenda kiliniki na wake zao ili waweze kufahamu maendeleo ya afya ya wake zao alisema Ngasa
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment