Home » » HATARII: WANAFUNZI WAKIKE WAKUTWA WAKIWA WAMEPOTEZA FAHAMU KWENYE BWENI LAO HUKU WAKIWA WAMECHANJWA CHALE

HATARII: WANAFUNZI WAKIKE WAKUTWA WAKIWA WAMEPOTEZA FAHAMU KWENYE BWENI LAO HUKU WAKIWA WAMECHANJWA CHALE


Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
Katika hari isiyotarajiwa  baadhi ya Wanafunzi Wasichana wa shule ya Sekondari ya Mpanda Ndogo Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi wamekutwa wakiwa kwenye bweni lao   walilokuwa wamelala huku wakiwa wamepoteza fahamu na miili yao kuchanjwa chale   bila wao kujitambua
 Tukio hilo la ajabu  lilitokea  usiku wa kuamkia jana shule hapo tukio ambalo limethibitishwa kutokea na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Bodi ya shule hiyo  iliyoko umbali wa kilometa 18 kutoka Mji wa   Pascal  Mnyongi  alisema kuwa  bweni hilo la wasichana lilikuwa na jumla ya wanafunzi 40 ambao walikuwa wamelala kwenye bweni hilo
 Alisema siku hiyo kabla ya tukio hilo wanafunzi hao wasichana  walikwenda kujisomea darasani kama ambavyo ilivyokuwa kawaida yao na walijisomea hadi majira ya saa nne usiku na kisha walirudi kwenye bweni lao na kulala
 Alieleza ilipotimia jana majira ya saa kumi na mbili na nusu asubuhi mwanafunzi  mmoja  wa kidato cha tatu aitwaye  Terezia Joseph  aliamka na kwenda  shule kwa lengo la kuwahi kupiga namba kwa ajiri ya kuhesabiwa kwa wanafunzi waliowahi  kufika shuleni hapo huku akiwa amewaacha wenzake wakiwa wamelala
Mwenyekiti  wa Bodi hiyo ya shule alieleza  Waalimu wa shule hiyo walishitushwa kuona muda unazidi kwenda huku wanafunzi waliokuwa wakilala kwenye bweni hilo wakiwa hawaonekani
  Waalimu hao waliamua kwenda kwenye bweni hilo ilikujua kilichokuwa kimewafanya wanafunzi hao washindwe kuwepo shuleni mida hiyo wakati sio kawaida yao
 Alisema waalimu hao walipofika kwenye bweni walijaribu kuwaita kwa kuwaamsha wanafunzi hao lakini hawakuweza kuitikia hari ambayo ilizidikuwashitua waalimu wao na kuamua kusukuma kwa nguvu mlango wa kuingilia ndani lakini walishindwa kufungua
Ndipo walipomwita mwanafunzi mwenza  Terezia  Joseph  ajaribu kuufungua mlango huo ambao ulikuwa umewashinda waalimu wake
 Alieleza ndipo  Terezia alipofika hapo na aliposukuma mlango huo ulifunguka  na kisha waalimu waliingia ndani ya bweni hilo na kuwakuta wanafunzi hao wasichana wakiwa wanagalala chini ya vitanda vyao huku wakiwa hawana fahamu na huku sehemu zote za miili yao ikiwa imechanjwa chale na mtu asiyefahamika
 Alisema  kati yao wanafunzi   12 hari zao zilikuwa ni mbaya hari ambayo  iliwalazimu kuwapeleka kwenye zahanati ya Jijiji cha Ifukutwa  na baada ya kupatiwa matibabu hali zao ziliendelea  vizuri na wameisha ruhusiwa kurudi nyumbani kwao
Mnyogi alisema  baada ya kutokea kwa tukio hilo bodi ya shule ilifanya kikao cha dharula na wazazi wa wanafunzi wanaosoma shuleni hapo na Mwenyekiti wa Waganga wa jadi wa Kata hiyo ya Mpanda Ndogo  kujadili hali hiyo  ambayo imekuwa ikitokea   mara kwa mara
 Alisema Mwenyekiti wa Waganga wa Jadi aliwaeleza  kuwa  kazi hiyo   ya kuzuia matukio hayo yasiendelee anaweza kuifanya  na kuondoa tatizo hilo kabisa shuleni hapo ila wanatakiwa wamlipe wazazi gharama kidogo ndipo wazazi wa wanafunzi walipochangishana na kufikisha kiasi cha shilingi Tsh 70,000 na kumkabidhi
 Alieleza mwezi januari mwaka huu  kulitpkea matukio  mawili kwenye bweni hilo ambapo tukio la kwanza  nguo zao  za ndani zilikutwa zimepangwa  chini kulingana na idadi ya wanafunzi wanaolala humo na tukio la pili wanafunzi hao walijikuta wakiwa wamefanya mapenzi bila wao kujitambua
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza  Mwamlima  amethibitisha kupokea kwa taarifa za tukio hilo la  kushangaza
 Amesema amesema anatarajia leo kufika shuleni  hapo na kufanya kikao na bodi ya shule , wazee maarufu ,na waganga wa jadi na viongozi wa madhehebu ya Dini mbalimbali kujadili hari hiyo
MWISHO
        


Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa