Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Mkuu wa Mkoa wa
Katavi Dr Ibrahimu Msengi amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Mlele Kanali Ngemela
Lubinga kupeleka wakaguzi kwenye shule za Sekondari kufuatilia matumizi ya fedha zilizotumika kwa ajiri ya ujenzi wa
majengo ya maabara ya shule za sekondari
katika Halmashauri ya Nsimbo baada ya kutoridhishwa na
ubora wa majengo hayo
Agizo hilo alilitowa hapo jana wakati alipokuwa
akitembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo ya maabara ya shule za sekondari za Halmashauri ya
Nsimbo Wilaya ya Mlele
Alisema katika majengo ya maabara aliyotembelea na kukagua hajaridhishwa na ubora wa majengo hayo hari
ambayo inatia shaka ya matumizi yaliyotumika ya fedha
za ujenzi wa maabarahizo
Dr Msengi alieleza inashangaza sana kuona
majengo ya serikali yanajengwa kwa
gharama kubwa zaidi kulikomajengo ya
watu binafsi na huku yakiwa
yamejengwa chini ya kiwango
Alisema majengo ya Serikali yamekuwa
yakijengwa ovyo kwa kuwa yamekuwa na usimamizi mbovu na matokeo yake yamekuwa
yakiharibika hata kabla ya kuanza
kutumiwa kutokana na kutosimamiwa ipasavyo kwenye kila hatua yanapokuwa
yanajengwa
Alifafanua majengo ya Serikali yamekuwa
yakijengwa chini ya kiwango huku viongozi wa
maeneo husika wakiwa wanaangalia
tuu kwa ajiri ya kuwaogopa wakandarasi
Wakati wa
wakandasi kufanya kazi zao kiujanja ujanja umekwisha wakandarasi wanamna hiyo watafute sehemu
nyingine yakufanyia kazi sio Katavi kwa
sasa
Pia
alisema kuwa amefuta ziara za
Madiwani wa Halmashauri ya Nsimbo ambayo walikuwa wamepanga kuifanya kwenye
baadhi hapa nchini iliwasimamie
maabara kwenye Kata zao hadi zikamilike
Rc katika zira hiyo alitembelea shule za
Sekondari za Kasokola , Kanoge , Mtapemda ,Nsimbo na Kenswa
zilizopo katika Halmashauri ya
Nsimbo na kugundua kasoro
mbalimbali kwenye majengo hayo
Miongoni mwa
kasoro hizo ni kuta za majengo kujengwa huku zikiwa zimepinda
madirisha na milango kutengenezwa
kwa mbao zisizofaa hari ambayo ilimlazimu
mkuu huyo wa Mkoa kuwaagiza
wakandarasi kufanyia marekebisho ya kasoro alizozigundua
Pia majengo hayo
yenye kasoro wakandasi wasipewe fedha
tena mpaka hapo watakapo kuwa wamerekebisha
na yeye atapita tena kuyakagua
majengo hayo ya maabara
Kwa upande Mkuu
wa Wilaya ya Mlele Kanali Ngemela Lubinga alieleza kuwa maagizo hayo yaliotolewa na
Mkuu wa Mkoa atayafanyia kazi mapema
iwezekanavyo
Inashangaza sana kuona
kila mkuu wa Idara katika Halmashauri anadigilii lakini wanashindwa kusimia vizuri shughuli za Halmshauri tofauti na watu
wenye elimu ya kawaida anatamani sana
Wakurugenzi wa Halmashauri zote hapa
Nchini wawe wanajeshi alisema Kanali Lubinga
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment