Home » » BARAZA LA MADIWANI LA HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA WAPENDEKEZA KUHAMIA TONGWE

BARAZA LA MADIWANI LA HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA WAPENDEKEZA KUHAMIA TONGWE


Na   Walter  Mguluchuma
Katavi
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi  wamepirisha pendekezo la  kuhamishia makao yao makuu  kutoka yaliko sasa Mpanda  Mjini  na kuhamia  katika eneo la Kijiji cha Majalila  Kata ya Ntongwe    Wilayani hapa
 uamuzi huo  ulipitishwa  jana  kwenye  kikao  cha   baraza maalumu la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda kilichofanyika kwenye ukumbi wa Idara ya maji mjini hapa   kikao hicho ambacho kiliongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Yassin Kiberiti kilichouzuriwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dr Ibrahimu Msengi
Halmashauri hiyo iliagizwa na Wizara ya  TAMISEMI  ihamishe makao  yao  yaliposasa mjini Mpanda na kuhamia  kwenye maeneo yao iliwawe  karibu na wananchi wao
 Awali  Baraza hilo la madiwani  walikuwa wamapendekeza  kuhamishia makao yao makuu katika  Tarafa ya Kabungu  eneo  ambalo lilikataliwa  kutokana  na sehemu hiyo kuwa karibu na Mji wa Mpanda
 Katika kikao hicho cha Baraza la madiwani  zilitolewa taarifa mbili  za timu ya wataalamu  ambapo moja iliteuliwa   na  Katibu Tawala wa Mkoa na nyingine iliteuliwa na  Halmashauri hiyo  ilikuangalia vigezo  vilivyo kuwa vimetolewa na TAMISEMI kuhusiana na sifa za mahari panapositahili  kuwa makao makuu ya Halmashauri   
 Mapendekezo hayo ya timu hizo za wataalamu  zilitofautiana wakati ile  timu ya wataalamu  walioteuliwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi  walipendekeza makao hayo yahamia katika katika eneo la  Kamikusu  kata ya Katuma umbali wa Kilometa  65 kutoka Mpanda Mjini wakati timu ya wataalamu  wa Halmashauri walipendekeza makao yao makuu yawe  katika Kijiji cha Majalila  Kata ya Ntongwe umbali wa kilimeta  23 kutoka Mpanda Mjini
Diwani wa kwanza kuchangia hoja alikuwa ni Diwani wa Kata ya Kabungu  Nassor Kasonso  ambae alipendekeza kuwa makao makuu ya Halmashauri hiyo  yahamie  Kata ya Ntongwe na sio kata ya Katuma  kwa kile alichoeleza kuwa eneo hilo  linazohuduma muhimu  za kibanadamu  kuliko Katuma
 Pia eneo hilo lipokaribu na barabara kuu  inayoelekea Mkoani Kigoma na eneo hilo lipo kwenye mpango wa kupatiwa umeme wa vijijini wa REA  na pia nikatikati
 Diwani wa Kata ya Mpanda Ndogo  Hamad Mapengo aliliambia Baraza hilo kuwa  kitendo cha kuhamishia makao makuu  kata ya Katuma kutaigharimu  Halmashauri hiyo fedha nyingi kwa vile  ardhi  ya maeneo hayo yanamilikiwa kihalali na wananchi  hivyo watalazimika  Halmashauri kuwalipa fidia watu hao  kwa ajiri ya ardhi yao
 Pia alisema  eneo hilo  ni sawa na kujenga Makao yao makuu porini kwani upo uwezekano wa wananchi  kutosogea kujenga makazi yao  karibu na makao makuu ya Halmashauri
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Katavi  Dr  Ibrahimu Msengi alisema lengo  la msingi kwa Halmashauri hiyo ni kuhama mjini na kuhamia kwenye eneo lao ili wawe karibu na wananchi wao kuliko ilivyo sasa
 Alieleza mapendekezo hayo walioyatowa  yatajadiliwa kwenye vikao vya juu na kabla ya kutolewa maamuzi ni lazima timu ya wataalamu  mbalimbali ifike kwenye maeneo hayo
MWISHO
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa