Home » » RC awapa somo wakandarasi‏

RC awapa somo wakandarasi‏


Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dr Ibrahimu Msengi  amewaeleza wenye Kampuni za ukandasi wanaofanya shughuli zao kati Mkoa huu kuwa atahakikisha  anathibiti  kila  kitakachokuwa  ninaendelea  kwenye ujenzi  wa miradi ya maendeleo  ili  aweze kubaini thamani  ya gharama ya ujenzi wa miradi   kama inalingana na thamani ya fedha
Kauli hiyo aliitowa hapo jana wakati alipokuwa akizungumza na wakandasi mbalimbali wa Mkoa wa Katavi pamoja na wataalamu  wa Halmashauri zote za Mkoa wa Katavi  kwenye ukumbi wa Idara ya Maji Mjini hapa
 Alisema Mkoa wa Katavi umekuwa na tatizo la miradi mingi ya ujenzi kujengwa chini ya kiwango kisicholidhisha kutoka na wataalamu kutowakagua kazi zao kwa wakati
Inashangaza kuona majengo yaliyojengwa mwaka 1971 yakiwa yamejengwa kwa kiwango kizuri   wakati  huo kulikuwa na zana duni za ujenzi lakini leo hii kuna zana bora za ujenzi  na makampuni mengi ya Wakandasi  majengo yamekuwa yanajengwa ovyo
 Alisema kuanzia sasa mkandasi yoyote atakae pewa kazi ya kujenga jengo la Serikali katika Mkoa wa Katavi  ahakikishe  anakuwa na mafundi wenye utaalamu wa kujenga  vinginevyo wakijenga ovyo  watalazimika  kuridia kujenga kwa gharama zao wenyewe na hawata lipwa
Alifafanua  ujenzi wa majengo kujengwa chini ya kiwango umekuwa ukisababishwa na wakandasi na wataalamu wa Halmashauri kutotimiza wajibu wao  wa kuwajibika  kuwasimamia wakandarasi
 Alisema  mkandarasi yoyote  ambae  anaona hawezi kujenga miradi  kwa kiwango  kinachositahili   atanyimwa  tenda ya kufanya kazi na ni bora akatafute sehemu nyingine ya kufanyia kazi
Vilele kwa wataalamu ambao wataonekana wakuwa wameshindwa kutimiza wajibu wao watachukuliwa hatua za kinidhamu za kiutumishi
Dr  Msengi  alikataa sababu  zinazowafanya wakarasi wachelewe kukamilisha miradi na kujenga  chini ya kiwango zilizotolewa kwenye kikao hicho na mwakilishi wao Nashon Petro  ambae alidai kuwa  kiwango cha fedha za ujenzi huwa zinakuwa ni ndogo na gharama ya  vifaa  vya jenzi ziko juu kutokana na mazingira ya huku hasa wakati wa masika
 Sababu nyingine ni  kucheleweshewa malipo yao kwa muda unaositahili kutokana na kuchelewa  kukaguliwa shughuli zao na wataalamu wa Halmashauri
  Madai hayo yalipingwa na Rc kwa kile alichoeleza kuwa  endapo  fedha zingekuwa ni ndogo  wasingekuwa wanachukua tenda ya ujenzi  kwani gharama hiyo huwa wanakuwa wanaifahamu kabla ya ujenzi


Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa