Home » » MPIGA DEBE WA MABASI JELA KIFUNGO CHA MAISHA KWA KOSA LA KUMLAWITI MTOTO WA KIUME MWENYE UMRI WA MIAKA SABA‏

MPIGA DEBE WA MABASI JELA KIFUNGO CHA MAISHA KWA KOSA LA KUMLAWITI MTOTO WA KIUME MWENYE UMRI WA MIAKA SABA‏

Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
 Mpiga  debe kwenye  stendi ya mabasi ya mji wa Mpanda Mkazi wa  Mtaa wa Mji wa Zamani  Wilayani  Mpanda Mkoa wa Katavi  Maiko   Edward (BAROTI) 25 amehukumiwa  kifungo cha maisha jela  baada  ya kupatikana na hatia ya kumbaka  mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka saba  mkazi wa mtaa wa Nsemlwa ambae jina lake tunalo
Hukumu  hiyo iliyovutia  hisia za watu wengi wa mji wa Mpanda   ilitolewa juzi na  Hakimu mkazi   Mfawidhi  wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda  Chiganga Ntengwa  baada ya mahakama kulidhika  na  ushahidi uliotolewa Mahakamani hapo wa pande mbili za mashitaka na utetezi
 Awali  akisoma   maelezo ya upande wa mashitaka  mwendesha mashitaka  Kurwa  Sikwesa  alidai Mahakamani hapo kuwa   mshitakiwa  Maiko Edward alitenda kosa hilo hapo  Oktoba  9 ,2014 majira ya saa kumi na mbili jioni katika eneo la mji wa zamani
 Alisema siku hiyo ya tukio  mshitakiwa  alikutana na mtoto huyo njiani  wakati  alikuwa akielekea nyumbani kwa  wazazi wake huko katika mtaa wa Nsemlwa  ndipo alipomshika mkono mtoto huyo na kisha kwenda nae kwenye pagala  la nyumba  lililokuwa katika mtaa wa  Mji wa  Zamani
 Mwendesha mashitaka alidai kuwa baada ya kufika kwenye pagala hilo la nyumba  mshitakiwa  alishikisha mkononi mtoto huyo kipande cha mbao na kisha aliingia ndani ya chumba kimoja kilichokuwa kwenye pagala hilo
 Alieleza  baada ya kuingia nae   ndani ya chumba hicho  mtuhumiwa alitowa kisu  na kuchoma kwenye ubao aliokuwa ameshika mtoto     huyo ikiwa ni ishara ya kumtishia  kisha alimwambia endapo atakata kulawitiwa au akipiga kelele atamuuwa kwa kumchoma na kisu kama alivyofanya  kuchoma kisu ubao huo
  Mwendesha  mashitaka alidai kuwa  ndipo mtuhumiwa  Maiko  Edwadr alipomvua mtoto huyo kaputula yake  na kisha  yeye  alivua saruali yake na kutowa uume wake na kuupaka mate na kisha kuanza kumlawiti mtoto huyo kwa nguvu  mpaka alipomaliza haja yake  
 Alidai mahakamani hapo  kuwa baada ya kumlawiti mtoto huyo alimtishia tena kuwa endapo atamwambia mtu  yoyote kitendo hicho alichomfanyia   atamuuwa hata hivyo mtoto huyo baada ya kufika kwa wazazi wake  alilazimika kuwaambia  kutokana na hari ya maumivu aliyokunayo
Wazazi wake  walimuuliza kama anaweza kuwa anamfahamu mtu aliyemfanyia kitendo hicho ndipo alimtaja kuwa ni  mtuhumiwa Maiko Edward ndipo  wazazi wake  na mtoto  walipokwenda kituo cha polisi cha  Wilaya ya Mpanda na kutoa taarifa kisha walimpeleka katika hospitali ya Wilaya ya Mpanda  ambapo kutokana na hari mbaya aliyokuwa nayo mtoto huyo alilazimika kulazwa
  Alisema  jitihada za kumtafuta mshitakiwa zilianza   ambapo siku moja mtoto huyo alipokuwa  amekaa nyumbani kwao akiwa na mama yake  alimwona mshitakiwa Maiko akipita karibu na nyumba yao na ndipo alipokimbia na kujifisha nyuma ya mgongo wa mama yake ambae alimuuliza anajificha nini na ndipo alipomjibu kuwa anamwogopo mshitakiwa  kwani alimwammbia wakati  anamlawiti  kuwa  atamuuwa
 Alieleza  ndipo mamayake  alipokwenda kituo cha polisi kutoa taarifa ya kuwa yule mtuhumiwa aliyekuwa anatafutwa  ameonekana  ndipo polisi walipofanikiwa kumkamata mtuhumiwa  akiwa kwenye eneo la stendi ya  mabasi aliko kuwa akifanyia kazi ya kupiga debe
Mshitakiwa  katika utetezi wake  mshitakiwa  aliomba mahakama imwachie huru  kwani   yeye hakutenda kitendo hicho  na wala alikuwa hamfahamu kabisa mtoto huyo aliyelawitiwa
 Baada ya utetezi huo Hakimu   Chiganga    Ntengwa allisoma hukumu hiyo kwa kueleza kuwa mahakama  bila kuwa na shaka yoyote imemuona mshitakiwa Maiko Edward  kuwa  amepatikana na hatia ya kulawiti mtoto  kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo  wa mtoto mwenyewe pamoja na Daktari
Hivyo mshitakiwa amepatikana na kosa  la kifungu cha sheria  namba(154) cha  kanuni ya adhabu  sura ya 16 marejeo ya mwaka  2009 kutona na  kosa  hilo  adhabu yake inatokana na kifungu cha  sheria   namba  235 sura ya 20  ya marekebisho ya mwaka 2009  kwa kwahiyo mahakama kuanzia jana imemuhukumu Maiko Edward kwenda jela kifungo cha maisha

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa