Katavi
Madiwani wa Halmashauri ya Nsimbo katika Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi ambao wanamaliza muda wao mwaka huu wameshauri kupimwa kwanza maambukizi ya VVU kabla ya kuchukua fomu za kugombea Udiwani kwenye Kata zao ili waweze kutambua afya zao na kujua kama watakuwa na nguvu za kutosha kuwatumikia wananchi wao kwa kipindi kijacho
Ushauri huo ulitolewa juzi na Diwani wa Kata ya Kapalala Reward Sichone kwenye kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Nsimbo kilichofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo
Sichone alisema ni vizuri kwa madiwani wa Halmashauri hiyo wanao maliza muda wao mwaka huu wakaandaliwa utaratibu na Halmashauri hiyo wa kupimwa maambukizi ya VVU kabla ya kumaliza muda wao wa uongozi mwaka huu
Alilieleza Baraza hilo la madiwani kuwa endapo watapimwa afya zao mapema itawafanya wajitathimini kabla ya kuchukua fomu za kugombea udiwani kwenye Kata zao za sasa
Sichone alisema endapo diwani atapimwa na kukutwa anamatatizo kwenye afya yake itamsadia kuona kama kweli atakuwa na uwezo wa nguvu za kufanya kazi za wananchi kwenye eneo lake
Aliwafafanulia kuwa haitakuwa vizuri kwa diwani ambae atakae pimwa na kukutwa na maambukizi ya VVU halafu achukue fomu za kugombea tena wakati anajua kuwa ana matatizo ya afya yake hari ambayo itamfanya kutokuwa na nguvu za kufanya kazi za wananchi wake hivyo swala la madiwani kupima afya zao ni jambo la msingi sana
Kwa upande mwenyekiti wa kamati ya kudhibiti ukimwi wa Baraza hilo la Madiwani Sylvester Nswima ambae pia ni Diwani wa Kata ya Sitalike alipinga ushauri huo wa Diwani Sichone
Nswima alilieleza swala hilo la madiwani wa Halmashauri hiyo kupimwa afya zao haiwezekani kwani kupima ni hiyari ya kila mtu na sio lazima
Nae Mwenyekti wa Halmashauri ya Nsimbo Mohamed Assenga alieleza kuwa kitendo cha wao madiwani kupima afya zao kinaweza kuwa ni mfano mzuri kwa watumishi wa Halmashauri hiyo na wananchi wa Halmashauri hiyo kuwaona viongozi wao wakimwa afya zao na kuwafanya nao waige
Alisema madiwani tusihofu kupimwa bali tuangalie utaratibu wa kuwaita wataalamu waje watupime afya ili tuwe mfano kwa watu wengine kwenye Halmashauri hiyo na Mkoa wa Katavi kwa ujumla wake alieleza Assenga
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment