Home » » HATARI SANA : MWANAMKE AUWAWA KIKATILI NA KISHA KUFUKIWA ARDHINI SHAMBANI KWAKE

HATARI SANA : MWANAMKE AUWAWA KIKATILI NA KISHA KUFUKIWA ARDHINI SHAMBANI KWAKE


Na  Walter  Mguluchuma
Katavi yetu blog
Mwanamke mmoja alifahamika kwa jina la  Minza  Mwanalushinge (26)  Mkazi wa Kata ya Kibaoni  Tarafa ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele  Mkoani Katavi ameuwawa kikatili  kwa kukatwa katwa  na mapanga  viungo  vyake na    na kisha mwili wake kufukiwa  chini ya ardhi shambani kwake
Kwa mujibu wa Kamanda  wa  Jeshi la  Polisi wa  Mkoa wa Katavi  Kamishina  msaidizi  mwandamizi  Dhahiri Kidavashari mauwaji hayo ya kikatili  yalitokea  hapo  juzi  majira ya saa moja asubuhi  huko  katika kijiji cha Manga Kata ya  Kibaoni
 Siku  hiyo ya tukio  marehemu  aliondoka  nyumbani kwake  majira ya saa kamili  asubuhi   kwenda kuchota  maji   kisimani  umbali wa kilometa moja kutoka nyumbani kwake alikokuwa akiishi na  mumewe aitwaye  Kimbulu  Joseph
 Kamanda kidavashari alisema  wakati  marehemu akiwa anarudi nyumbani huku  akiwa amebeba ndoo yake ya maji  ndipo alikutana na watu wasio fahamika  ambao walimshambulia kwa mapanga   katika sehemu mbalimbali za mwili wake
 Alieleza  baada ya kuwa wamemshambulia marehemu  hadi kufa wauwaji hao walianza kukatakata  viungo vya  mwili wa marehemu  kwa   kukata miguu yake  na mikono  kwa kuitenganisha  na mwili wa marehemu
 Kidavashari alisema  kisha wauwaji hao waliuburuza mwili wa marehemu kutoka kwenye eneo hilo  walilofanyia mauwaji hadi shambani kwa marehemu
 Alieleza   kisha wauwaji hao  baada ya kuwa wameufikisha mwili huo wa marehemu kwenye   shamba lake  huku wakiwa wamekata viungo vya mwili wake  walichimba shimo na kisha walimfukia marehemu ardhini pamoja na viungo vya mwili walivyokuwa  wamevikata na kisha kutokomea  kusiko julikana
Kamanda Kidashari alisema  watu waliopita  kwenye eneo la   karibu na tukio  walishitushwa kuona ndoo ya maji ikiwa imetupwa kichakani  huku kukiwa hakuna mtu aliyeonekana  kwenye eneo hilo zaidi ya  damu zilizokuwa zimetapakaa hari ambayo iliwafanya waende  kutoa  taarifa kwa   viongozi wa serikali wa kijiji hicho ambao nao walitowa taarifa kwenye kituo cha polisi cha Kibaoni
Polisi wa kituo cha Kibaoni walifika kwenye eneo hilo  na ndipo walipokuta kuna mbuluzo ambao walilazimika kuufuata hadi uliko ichia kwenye shamba la marehemu na ndipo walipoweza kuona kuna kitu kinaonekana kufukiwa ardhini na walipofukua eneo hilo waliweza kuukuta mwili wa marehemu ukiwa umefukiwa ardhini  huku ukiwa umekatwa miguu na mikono yake  ambavyo vyote  vilikuwa  vimefukiwa kwenye shimo hilo pamoja na mwili wake
 Kidavshari ameeleza kuwa jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi mpaka sasa   ilina washikilia  watu wawili  kwa tuhuma za kuusika na mauwaji hayo ambao  ni  Kimbulu  Joseph(52) ambae ni mume wa marehemu  na Joseph  Abel (35) mkazi wa  Kitongoji cha  Vilolo Kata ya Kibaoni Wilaya ya Mele
 Watuhumiwa wanatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote mara baada ya uchunguzi utakapo kuwa umekamilika ili waweze kujibu tuhuma zinazowakabili
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa