Home » » HATARI: ASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA KUMUUWA BABA YAKE MZAZI KWA IMANI ZA KISHIRIKINA

HATARI: ASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA KUMUUWA BABA YAKE MZAZI KWA IMANI ZA KISHIRIKINA


Na  Walter  Mguluchuma
Katavi yetu Blog
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi linamshikilia mtu mmoja  aitwaye  Kanedeku Giti (26) Mkazi wa  Kijiji cha  Minyoso  kata ya Kibaoni  Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi  kwa tuhuma za kumuuwa  baba yake mzazi aitwaye  Giti  Mawiti (53) kwa kumpiga na kitu kizito kichwani  kutokana  imani za kishirikina akimtuhumu marehemu kumuuwa mtoto wake  kwa ushirikina
Kamanda wa Jeshi la polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri  Kidavashari  alisema mbele ya waandishi wa habari ofisini kwake  kuwa tukio hilo lilitokea hapo  jana majira ya saa tatu  na robo usiku nyumbani kwa marehemu
 Alisema kabla ya tukio hilo marehemu alikuwa nyumbani kwake  huku akiwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kuumwa tumbo lake  ambapo baada  ya kuona maumivu yanazidi kuwa makali  alilazimika  kuwaamsha watoto wake watatu ambao alikuwa akiishi nao  ambao ni  Kadeku   Giti  (26) Tupindo  Giti (21)na   Nyanzobe Giti (16) ili wamchemshie maji ya kunywea dawa
 Alieleza  baada ya kuwa amewaamsha  watoto wake na kuwaagiza wamchemshie maji ya kunywea  dawa  Marehemu  aliamua k utoka  chumbani kwake na kulala sebuleni wakati akiwa  anaendelea kusubilia maji ya kunywea dawa ya kienyeji  yachemke
  Kamanda Kidavashari  alisema ghafla  alitokea  mtu mmoja huku akiwa    amewasha toshi  yenye mwanga mkali  ambayo iliwamulika machoni  na kuwafanya watoto wa marehemu  wa kimbie mbio kwenda kujificha  kichakani huku wakiwa wamemuacha baba yao akiwa amelala  sebuleni
 Wakati watoto wa marehemu wakiwa mafichoni baada ya muda mfupi walisikia  baba yao   akipiga mayowe ya kuomba msaada kwa watoto wake  lakini kutokana na hofu waliokuwa nayo  walishindwa kurudi  kutoa msaada kwa baba yao
Kamanda Kidavashari alisema baada ya kuona  hari imekuwa kimya  watoto wa marehemu waliamua kurudi nyumbani  na walimkuta baba yao  akiwa anagalagala  chini  huku  akiwa  amepigwa na kitu kizito kichwani    akiwa anakoroma
 Ndipo mtoto wake  Kadeku   Geti alipomuinua na kumbeba na kumpeleka chumba kwake  na kumlaza kitandani hata hivyo baada ya muda si mrefu akwa amefariki Dunia
 Alifafanua uchunguzi wa awali  umeonyesha kuwa  kulikuwa   chanzo cha  mauji  hayo ni kutokana na   ugomvi wa mara kwa mara baina ya  marehemu na  mwanae  Kanedeku Giti  ambae alikuwa akimtuhumu  baba yake kuwa alimuuwa mtoto wake  kwa  imani za kishirikina
 Alisema Polisi wanaendelea kumshikilia mtuhumiwa  Kanedeku Giti na upelelezi  bado unaendelea  na mara utakapo kamilika  mtuhumiwa atafikishwa mahakamani wakati wowote
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa