Na  Walter 
Mguluchuma 
Katavi 
jumla ya watoto
52 wenye umri wa chini ya miaka mitano wameferiki Dunia Wilayani Mpanda Mkoani
Katavi  katika  kipindi cha miezi sita cha kuanzia  Januari 
2014 hadi juni  mwaka huu kutokana
na sababu mbalimbali  ikiwepo upungufu wa
damu 
 Haya yalielezwa hapo jana na Muuguzi mkuu wa
Wilaya ya Mpanda Pius Buzumalle wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa
habari ofisini kwake 
 Alisema 
jumla ya watoto 52 wenye umri wa chini ya miaka mitano wamefariki
Wilayani Mpanda kutokana na  maradhi
mbalimbali  yalisababisha vifo vya watoto
hao 
Alifafanua katika
mwezi  Januari  watoto 19 walifariki Dunia  kutokana na ugonjwa wa  malaria kupanda  kichwani 
kuishiwa maji mwilini  baada ya
kuharisha  na kuishiwa damu 
Alisema  mwezi Februari  walifariki Dunia  watoto 15 
kutokana na ugonjwa wa malaria  
kuishiwa damu  na kutokana  maambukizi 
kwenye damu 
Mwezi   machi walifariki  watoto 
wanne vifo  ambavyo   vilisababishwa na  kuishiwa maji 
baada ya kuharisha  mfululizo  kwa muda mrefu 
na kuishiwa  damu mwilini 
 Muuguzi Mkuu Pius  Bumamalle alieleza  kuwa mwezi Aprili  walifariki watoto  nane vifo ambavyo   sababu 
za vifo hivyo vilitokana na 
malaria kupanda kichwani , upungufu wa damu  na 
kuishiwa maji mwilini 
 Alisema 
mwezi mei na  mwezi june
walifariki watoto sita vifo ambavyo 
vilisababishwa  na upungufu wa
damu na maji mwilini  ,kuharisha  na malaria kupanda kichwani 
 Alieleza  
kuwa Idara ya Afya katika Wilaya ya Mpanda inaendelea na mikakati
mbalimbali ya  kuokowa vifo vya watoto na
mama zao 
 Aliitaja baadhi ya mikakati hiyo ni   wanaendelea kuwaelimisha wazazi kwa kuwahamasisha  kuwapeleka watoto wao Hospitalini pindi tuu wanapo kuwa wamegua  na pia 
kuhakikisha wanawapeleka watoto wao kwenye  kiliniki 
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
0 comments:
Post a Comment