Home » » HATARI SANA: BODABODA AUWAWA KWA KUCHOMWA NA KISU NA KISHA KUPOLWA PIKIPIKI YAKE

HATARI SANA: BODABODA AUWAWA KWA KUCHOMWA NA KISU NA KISHA KUPOLWA PIKIPIKI YAKE


Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
 Mwendesha  pikipiki(BODABODA) aliyejulikana kwa  jina la Zakaria  Lungwa(24) mkazi wa  Mtaa wa  Kawajense Madukani  Wilayani  Mpanda Mkoani hapa  ameuwawa  kikatili  kwa kuchomwa na vifu tumboni  na watu wawili  ambao alikuwaakiwafafamu kwa sura  na kupolwa pikipiki yake
 Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari  alisema mauwaji ya kikatili ya Bodaboda huyo yalitokea hapo jana  majira ya saa  saba na robo usiku katika mtaa wa  Nselwa Kichangani  mjini Mpanda
 Alisema  siku hiyo ya tukio  marehemu  alikuwa na pikipiki yake  ina ya Sanya  yenye rangi nyekundu  yenye namba za usajiri  T.752 CQS  akiwa huko kwenye  maeneo ya  Night  Club ilyoko mtaa wa Madini akiwa  kwenye shughuli zake  za kila siku
Akiwa kwenye eneo hilo la Night Club  marehemu  alipata mteja mmoja  wa kiume   ambae  alimbeba kwenye pikipiki yake  na kuelekea  Mtaa wa Nsemlwa Kichangani
 Kamanda Kidavashari alieleza  walipofika  katika eneo la Mtaa wa Nsemlwa Kichangani  mteja yule  aliyempakia  alimuamuru marehemu  asimame  katika eneo ambalo hata alikuwa na nyumba yoyote hapo
 Ghafla katika eneo hilo alitokea mtu mwingine  mwanaume  na  alianza kumwambia marehemu ashuke kwenye pikipiki yake  na kisha alimvuta chini pembeni ya barabara
 Alisema baada ya kuona hari hiyo marehemu  alipiga mayowe ya kuomba msaada kwa majirani wa eneo hilo  hata hivyo hakuweza kupata msaada wowote kutoka kwa majirani wanaoishi kwenye eneo hilo
Mmoja wa  kati ya  watu watu  wale wawili  alitoa kisu  na kisha alimchoma marehemu tumboni  na kisha marehemu alianguka chini  na watu hao walichukua pikipiki  na kisha walitokomea kusiko julikana huku wakiwa wamemuacha marehemu akiwa anagalagala chini akiwa anatokwa na damu
Kamanda Kidavashari alisema  marehemu alipata msaada wa kupelekwa hospitali   ya  Wilaya ya Mpandabaada ya mtu mmoja aliyekuwa akpita kwenye eneo hilo akiwa na gari lale alipomwona marehemu akiwa anagalagala pembeni ya barabara
 Alisema marehemu baada ya kufikishwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda  alianza kupatiwa matibabu na wakati akiwa anaendelea kupatiwa matibabu   ambapo  ilipofikia  majira ya saa kumi na mbili jioni alifariki Dunia
Kidavashari alieleza Jeshi la Polisi   linamshikilia  mtu mmoja  anaejulikana   kwa jina la K halid  Seif (24) Mkazi wa  Mtaa wa  Nselwa  kuhusiana na tukio hilo ambae anadaiwa  kuwa  alionekana katika eneo hilo la Night C lub akiwa na mteja  aliyeondoka na marehemu
Alisema hata hivyo jeshi la polisi  linaendelea  na upelelezi  ilikubaini  watuhumiwa  wa  walihusika na mauwaji hayo ya kikatili
Kamanda Kidavashari ametowa wito  kwa madreva wote  wa Bodaboda wa  wa Mkoa wa Katavi  wanapoona  kumekuwa usiku  kama wamepata mteja  basi  wawe  wanakuwa madreva  wawili  wanaongozana   ili  kuweza  kusaidiana  kama  kutatokea  tatizo lolote
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa