Home » » HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA KUTUMIA TSH MILIONI 680 KWA HUDUMA YA MTANDAO WA BARABARA

HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA KUTUMIA TSH MILIONI 680 KWA HUDUMA YA MTANDAO WA BARABARA


Na  Walter Mguluchuma
Katavi
Halmashauri ya  Wilaya ya Mpanda Mkoani  Katavi  inategemea  kutumia  jumla ya  shilingi milioni  680,250,000 kwa ajiri ya  kufanya matengenezo  ya barabara zake  zenye  urefu wa  Kil0meta  73 ambaz0 ni sawa na  asilimia  17.7 ya mtanda wa barabara za Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda
 Hayo yalielezwa  hapo jana kwenye kikao cha baraza la   madiwani wa Halmashauri hiyo  na  mwenyekiti wa kamati ya  uchumi  ujenzi na mazingira  Diwani Hamad Mapengo
 Alisema katika kipindi cha mwezi  julai mwaka huu wa 2014  hadi  mwezi septemba 2014 Halmashauri hiyo imeendelea  kuzifanyia matengenezo  barabara  mbalimbali  za Halmashauri hiyo
Mapengo  alizitaja barabara hizo kuwa ni  ujenzi wa daraja la  mto  Itunya  upo  katika asilimia 50 ya utekelezaji  na utekelezaji bado unaendelea  na ujenzi wa daraja  la mto Kafisha  ambao tayari umeisha kamilika
Alifafanua Halmashauri ya  Wilaya ya Mpanda  inazobarabara za  kiwango cha  changalawe zenye  urefu wa kil0meta 172 na  na  barabara za udongo ni kilometa  239.9
 Alisema  kutokana na  barabara hizo kuwa nyingi ni zaudongo  wakati wa masika  uharibika  na hivyo  kupelekea usumbufu mkubwa  kwa watumiaji
Mapengo alitaja  changamoto nyingine kuwa ni  bejeti inayotolewa na  serikali   ni ndogo hivyo haikidhi  kuhudumia mitandao ya barabara  zilizopo katika Halmashauri ya  Mpanda
 Alitaja  changamoto nyingine kuwa ni fedha  za mfuko wa  barabara  zinafika kwa kuchelewa  na hivyo  kupelekea  kazi  kutokamilika kwa wakati  katika mwaka wa fedha  uliopangwa
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa