Home »
» MAADHIMISHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI KITAIFA KUIDHIMISHWA KATAVI KUANZIA AKTOBA 13 HADI OKTOBA 16
MAADHIMISHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI KITAIFA KUIDHIMISHWA KATAVI KUANZIA AKTOBA 13 HADI OKTOBA 16
Na Walter Mguluchuma
Mpamda Katavi
Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniaani ambayo hufanyika kila mwaka Oktoba 16 yamepanga kuadhimishwa Kitaifa Mkoani Katavi kuanzia Oktoba 13 hadi hadi oktoba 16 katika uwanja wa Kashaulili mjini Mpanda
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dr Rajabu Rutengwe wakati alipokuwa akitowa taarifa ya maadhimisho ya hayo hapo jana mbele ya waandishi wa ofisini kwake
Alisema katika kuadhimisha siku hiyo Mkoa wa Katavi umefanya maandalizi ya kutosha ilikuweza kuwaonyesha wananchi mbalimbali yale yanayofanyika katika sekta ya kilimo mifugo ,nyuki na ushirika
Dr Rutengwe alisema kwenye maadhimisho hayo kutakuwa na maonyesho ya badhaa mbalimbali zinazohusiana na sekta ya kilimo
Alifafanua wageni watakao toka nje ya Mkoa wa Katavi watapata furusa ya kutembelea miradi mbalimbali ya sekta ya kilimo kwa lengo la kujifunza yanayofanyika katika Mkoa wa Katavi na iliwaweze kutowa ushauri wa namna ya kufanikisha zaidi utendaji wa kazi katika sekta ya kilimo katika Mkoa wa Katavi
Mkuu wa Mkoa Dr Rutengwe alieleza kwenye maadhimisho hayo kutakuwa na kongamano na kilimo litakalo jadili masuala ya Hifadhi ya mazao ,uongezaji wa thamani ya mazao,uboreshaji wa kuku wa asili na utunzaji wa mazingira pamoja na uboreshaji wa lishe katika Mkoa wa Katavi
Aliwataka wakazi wa Mkoa wa Katavi kuitumia furusa hii ipasavyo kwa lengo la kujifunza na kuhakikisha yale watakayojifunza wayatumie vizuri na kwa usahihi zaidi ili kuweza kubadilisha hali ya kilimo na maisha kwa ujumla
Kauli mbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu ni kilimo cha Kaya lisha Dunia tunza mazingira hivyo Mkuu huyo wa Mkoa ametaka kaulimbiu hii iende sambamba na kauli mbiu ya Mkoa wa Katavi isemayo Katavi bila umasikini inawezekana
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment